Wanajeshi
wa kulinda amani wa Liberia waelekea Mali
Liberia imetuma wanajeshi karibu 50 huko Mali watakaojiunga na kikosi
cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo. Kwa mara ya kwanza baada ya kumalizika vita vya ndani vya miaka 14, Liberia imetuma wanajeshi hao wa kulinda amani huko Mali ambao watatekeleza kazi ya kulinda amani katika fremu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa.
Wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa Mataifa zaidi ya elfu 12 wanatazamiwa kuwasili nchini Mali kuanzia mwezi ujao ili kuchukua nafasi ya vikosi vya Ufaransa vilivyoko nchini humo. Kikosi hicho cha walinda amani kitakuwa na majukumu ya kurejesha amani na uthabiti nchini humo. Rais Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia amewataka wanajeshi wa nchi hiyo waliotumwa Mali kuheshimu sheria na kuwa na nidhamu katika muda wote wakataokuwepo huko Mali katika shughuli za kulinda amani.
CHANZO: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment