Wednesday, February 12, 2014

CHINA YATUMA CHOMBO CHA KWANZA MWEZINI



China yatuma chombo chao cha kwanza kwenda Mwezini
China, leo Imerusha chombo chao cha kwanza Kabisa kwenda mwezini.
Chombo hicho chenye jina Yutu kimerushwa kwa kutumia Rocket yao inayoitwa Chang’e Moon Lander. Safari hiyo ndefu imeanza leo (Jumatatu) saa saba nusu kwa mida ya huko.


Kama Safari hiyo ikienda vizuri bila matatizo, Chang’e itatua kwenye ardhi ya Mwezi katikati ya Mwezi huu Desemba.
Chombo hichi kitakuwa cha kwanza kutua kwenye mwezi kwa zaidi ya miaka 37, kwani chombo cha mwisho kutua kwenye mwezi kilitua mwaka 1976, na kilitumwa na wa-Soviet.
Bwana Zhang Zhenzhoung ambaye ni mratibu wa “Xichang Satellite Launch Center” anasema: “Kurushwa kwa Roketi hii ya Chang’e iliyobeba chombo Yutu kwenda mwezini kunaudhihirishia Ulimwengu Uwezo wa nchi Kubwa ya China”, akaendelea kusema: “Tushirikiane pamoja katika Utafiti wa Anga na kutimiza ndoto za China” alipokuwa akihojiwa na Chombo cha Televisheni cha CCTV.


Kama nilivyosema awali Chang’e inatarajiwa kutua Mwezini by Desemba 14 au 15, na kuanza kufanya tafiti mbalimbali za Ki-Sayansi kwenye Mwezi.
Mission hii ambayo ni ya kwanza kufanywa na nchi ya China ipo chini ya programu yao inayoitwa China’s Lunar Exploration Program ambayo inahusisha awamu kuu tatu ambazo ni: 1. Kuuzunguka Mwezi, 2. Kutua kwenye Mwezi, na 3. Kurudisha sampuli za mawe ya Mwezini Duniani ifikapo mwaka 2020.
Awamu ya kwanza ambayo ni Kuuzunguka Mwezi walishaikamilisha pale walipotuma Vyombo vyao vya Chang’e 1 na Chang’e 2 mwaka 2007 na 2010…
Na hii sasa ndio Awamu ya pili, ambayo ni” Kutua kwenye mwezi…


Kutana na YUTU:
Chombo hiki Yutu ambacho ndo kinatumwa Mwezini kina Uwezo wa kutua kutoka angani na kisha kutembea kama gari (Rover)
Kinatarajiwa kutua eneo katika Mwezi linaloitwa Sinus Iridum au “Bay of Rainbows”.
Chombo hicho kina matairi sita na kina kilo 140.
Jina “Yutu" kina maana "Sungura Aliyetukuka", na kwa tamaduni zao, Yutu alikuwa ni mfugo Kipenzi wa "Chang’e" ambaye ni "mungu aishiye mwezini". Jina hilo liliteuliwa kwa kura zilizopigwa na raia wa China.
Chombo hicho kitatembea kwenye mwezi kwa muda wa miezi mitatu, kikiendeshwa na Kuongozwa na wanaSayansi hapa Duniani.
Chombo hicho kimefungiwa Rada (radar) ili kusoma kwa karibu zaidi muundo wa Mwezi.
Kutua Kwenye Mwezi:
WanaSayansi wanasema ile hatua ya kutua kwenye Ardhi ya mwezi ndio itakuwa ngumu zaidi kwenye Safari hiyo.
Ma-Injinia waliokitengeneza wanasema, kitachukua takribani sekunde 700 mpaka kutua kwenye ardhi laini ya Mwezi.
Chombo kimefungiwa sensor zinazosoma mwendo wa Chombo na mazingira yanayokizunguka, pamoja na Injini ambayo imetengenezwa kupunguza mwendo wa Chombo hicho kadiri kitavyokuwa kikishuka kwenye ardhi ya Mwezi.
Chombo pia kimefungiwa Camera zenye mionzi mikali ya UltraViolet ambayo itakuwa ikielekezwa Duniani ili kusoma muundo wa “plasmasphere” ya Dunia. Pia kimefungiwa Teleskopu (telescope) kwa ajili ya Tafiti mbalimbali za Ki-Astronomia.
Katika mahojiano na CCTV, bwana Ouyang Ziyuana, ambaye ni mshauri mkuu wa Project hiyo, amesema; Chombo kitatulia kwanza kama mita 100 kutoka Mwezini. Halafu kwa kutumia camera zake maalum, kitachunguza mazingira, na kutafuta sehemu nzuri tambarare ili kitue. Halafu kinapoanza kutua; kikifika mita 4 kutoka kwenye ardhi ya mwezi, Injini yake itasimama; halafu kitaikunjua miguu yake ambayo ni imara, na hatimaye kutua kwenye Ardhi.
CHANZO: http://tuongeescience.


No comments:

Post a Comment