Thursday, February 13, 2014
MELI USS SAMUEL ROBERTS YATUA DAR ES SALAAM
Ile meli vita ya Marekani ambayo ilifumuliwa na wapiganaji wa Iran mwaka 1988 ya USS Samuel B. Roberts (FFG-58) imetia nanga nchini tokea majuzi.
Meli hiyo ya daraja la Oliver Hazard Perry yenye makombora (FFG) ndiyo iliyosababisha kuwapo kwa mashambulio dhidi ya Iran katika kile kilichoitwa Operation Praying Mantis.
Melivita hiyo ipo nchini katika mpango wa kushirikiana na Tanzania na nchi nyingine zinazopambana na uharamia za Mafunzo na Ushirikiano.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mara baada ya kutembelea meli hiyo, kamanda wa meli hiyo, Angel Cruz, alisema lengo la safari hiyo ni kuhamasisha ushirikiano kwa njia ya mafunzo dhidi ya uharamia.
“Tupo hapa kutoa mafunzo ya namna ya kutumia meli kama hii ya USS Samuel B. Roberts kupambana na uharamia, lakini pia tutajifunza kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),” alisema Kamanda Cruz.
Meli hiyo iliyopewa jina la Samuel B. Roberts, mpiganaji wa jeshi la majini la Marekani ambaye aliuawa wakati wa kutoa msaada kwa askari wa Marekani wakati wa vita vya Guadalcanal mwaka 1942 ni meli ya tatu kubeba majina ya wale waliofia wamarekani wenzao.
Meli hii ilizinduliwa Desemba 1984 na na kuingia mzigoni Aprili 1986 chini ya amari ya kamanda Paul X. Rinn.
Meli vita hii ambayo nyumbani kwake ni Newport, Rhode Island iliondoka kushiriki operesheni Operation Earnest Will Januari 1988 huko Ghuba ya Uajemi kazi yake kubwa ikiwa ni kusindikiza meli za mafuta za Kuwait wakati wa vita vya Irak na Iran.
Lakini Aprili 14 meli hiyo ilipamia bomu la kutegwa majini (M-08).
Bomu hilo lilitengeneza tundu la mita tano na kusababisha maji kujaa katika chumba chake cha injini. Wapiganaji walipambana na moto pamoja na kujaa kwa maji kwa saa tano na kuiokoa meli hiyo.
Juni 27, 1988, Roberts ilipakiwa ndani ya meli kubwa Mighty Servant 2, inayomilikiwa na kampuni ya Kiholanzi ya Wijsmuller hadi bandari ya Newport kwa gharama ya dola milioni 1.3.
Ilifikishwa katika yadi ya matengenezo ya Portland, Maine, Oktoba 6 , 1988 kwa matengenezo makubwa. Engine room iliondolewa yote na kuwekwa kitu kingine cha tani 315 na kuingizwa baharini tena kWa majaribio Aprili 1, 1989.
Baada ya miezi 13 ya marekbisho, Roberts ilirejea wajibu wake Octoba 16, 1989 .
Roberts iliingia katika operesheni Desert Storm mwaka 1990 na Operation Desert Shield.
Kwa sasa melivita hii inashiriki katika ulinzi wa Bahari ya Sham katika pata shika la kimataifa la kuhami mlango bahari huu ambao umevamiwa na maharamia wengi wao wakiwa wa Kisomali.
Kwa sasa hivi "Sammy B", kama inavyojulikana kiutani nyumbani kwake hasa ni Mayport,
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment