Wanajeshi
saba wa Tanzania, ambao ni miongoni mwa kikosi cha Umoja wa Mataifa, cha
kulinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanadaiwa kuwa wameuawa.
wanajeshi wa Tanzania waliojeruhiwa Darfur wakiwa katika matibabu |
Kwa mujibu
wa taarifa hizo, miili yao wanajeshi hao bado ipo nchini Sudan ikisubiri
taratibu za kusafirishwa kuletwa nchini.
Hii ni mara
ya kwanza kuripotiwa kwa idadi kubwa ya wanajeshi wa Tanzania wanaolinda amani
katika nchi mbalimbali kufa kwa wakati mmoja.
Agosti
mwaka jana wanajeshi watatu wa Tanzania huko Darfur waliripotiwa kuuawa kwenye
tukio kama hilo.
Msemaji wa
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) , Kanali Kapambala Mgawe
alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.
alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu vifo vya wanajeshi wa Tanzania huko Darfur, alisema kuwa naye amesikia, lakini hana taarifa rasmi kwa mujibu wa taratibu za kiofisi.
Hii ni mara
ya pili kwa wanajeshi wa Tanzania kuuawa katika Jimbo la Darfur, ambapo Agosti
mwaka jana, Kanali Mgawe alinukuliwa na vyombo vya habari akithibitisha kutokea
kwa vifo vya askari watatu ambao gari lao lilizolewa na maji walipokuwa
wakivuka mto uliokuwa umefurika maji.
Kanali
Mgawe aliwataja askari hao kuwa ni Sajini Julius Chacha, Sajini Anthony Daniel
na Koplo Yusuph Said na kwamba askari wengine walinusurika baada ya kuogolea.
Tanzania
ina askari 850 kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani jimbo la
Darfur, ambao ni sehemu ya askari 1,081 wa kulinda amani katika jimbo la
Darfur.
Aprili
mwaka huu Tanzania ilipeleka wanajeshi wa kulinda amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Congo (DRC), kupambana na kikundi cha waasi wa nchi hiyo M23 kinachopigana
kuiangusha serikali ya DRC.
No comments:
Post a Comment