FIDEL CASTRO; mwanamapinduzi
aliyepitia tabu nyingi katika kuwakomboa Wacuba
Mfumo
wake wa uongozi uliwakimbiza baadhi ya wasomi kwenda kuishi uhamishoni nchini
Marekani,
·Alimhenyesha dikteta Batista
na kufungwa jela miaka 15,
·Aungana na Ernesto ‘Che’
Guevara kusambaza mapinduzi ulimwenguni akianzia nchini Ghana, Algeria na
baadae Angola.
Fidel Castro, ameingia madarakani mwaka 1959 baada ya mapinduzi ya
mwaka huo ambayo yalimuondoa madarakani dikteta Fulgencio Batista na kuwa
waziri mkuu wa Cuba mwaka 1961 na baadaye akaghairisha uchaguzi mkuu wa nchi
hiyo na pia kuipinga katiba ya nchi hiyo.
Casrto ameiongoza nchi ya Cuba bila kuongozwa na katiba ya nchi hiyo iliyoandikwa mwaka 1940 mpaka mwaka 1976, ambapo taifa hilo lilitunga katiba mpya ambayo iliruhusu ukomo wa upigaji kura wa Cuba. Baadae mwaka huo wa 1976, Casrto alichaguliwa na bunge la nchi hiyo kuwa rais wa nchi ya Cuba.

Baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Cuba, Castro akaanza taratibu
kuingoza nchi hiyo katika misingi ya kijamaa, baada ya kubadilisha mifumo ya
kijamii na kiuchumi.
Alianzisha pia programu mbalimbali zilizolenga kuongeza idadi ya wasomi katika nchi na kugawa huduma bora za afya kwa kila raia.

Mfumo wa siasa za kijamaa wa serikali ya Cuba, uliwafanya wasomi
wengi na watu wa fani mbalimbali kuishi uhamishoni. Hali hii ilitokana pia na
mfumo wa serikali wa kukamata biashara, kuondoa chaguzi mbalimbali,
kuanzisha mfumo wa kijeshi wa kijamii, kuongoza vyombo vya habari pamoja na sera ya elimu, kulipelekea watu wengi wasiopenda mabadiliko kuhamia uhamishoni katika nchi za Uhispania, Mexico, Ufaransa na Marekani.

Katika kipindi cha vita baridi, Casrto alijiingiza katika ujamaa
hasa uliokomaa ambao ulikuwa unaongoza na Umoja wa nchi za kijamaa (USSR) ili
kuongeza na kuyapa nguvu mapinduzi ya kujikomboa kwa nchi za Amerika ya kusini
na afrika.
Katika hili Castro na harakati zake za kijamaa walipata upinzani kutoka Marekani, nchi ambayo ilikuwa rafiki mkubwa na mshirika mkubwa wa kibiashara na cuba.

Marekani iliona kuendelea kufanya biashara na nchi ya Cuba
isingekuwa jambo jema kwani nchi ya Cuba ilikamata mali za marekani, hivyo
wanasiasa wengi wa Marekani waliona siasa za kijamaa za Castro na kujiunga
kwake na umoja nchi za Kisovieti ni tishio la usalama kwa Marekani.
Alikotokea Fidel Castro
Fidel Aljandro Castro Ruz, amezaliwa katika kitongoji kikubwa
kilichopo karibu na mji wa Birani katika jimbo la Oriente, nchini Cuba, akiwa
ni mtoto wa tatu kuzaliwa kati ya watoto saba.
Wazazi wa Castro walikuwa ni wahamiaji kutoka nchini Uhispania. Alianza elimu yake katika shule ya umma iliyopo karibu na mji wa jirani na kwao wa Mayari.
Akiwa shuleni hapo Castro aligundulika kuwa ana kipaji cha kusoma na kutokana na hilo Castro akawa anafundishwa binafsi na baadaye akaandikishwa katika shule ya La Salle iliyoko katika mji wa Santiago de Cuba, ambayo ilikuwa anaendeshwa na makasisi wa kifaransa.
Baadae akajiunga na shule binafsi ya kanisa katoliki ya Doleres Colegio, ambayo ilikuwa inasifika kwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, lakini pia kiwango cha elimu iliyokuwa inatolewa kilikuwa cha hali ya juu.

Mwaka 1940, Castro alijiunga na shule ya sekondari ya Belen iliyopo
mjini Havana, ambako alijifunza historia ya Cuba na kumsoma mwasisi wa taifa
hilo ambaye alikuwa mpiganiaji wa uhuru wa Cuba kutoka kwa Uhispania.
Mwaka 1945, Castro alijiunga na skuli ya sheria katika chuo kikuu cha Havana, ambapo ilimpa fursa ya kujihusisha na masuala ya siasa ambapo alijiunga na chama cha watu wa Cuba (Party of Cuban people) ambacho kilikuwa kinakosoa kwa wazi serikali ya rais wa wakati huo Ramon Grau San Martin na kulazimisha mabadiliko katika mfumo wa uendeshaji wa serikali hiyo.

Chama hicho kilitaka serikali ijenge umoja wa kitaifa miongoni mwa
Wacuba, pia kupinga ushawishi mkubwa kutoka mataifa ya kigeni katika mambo ya
kijamii, kupendelea zaidi usawa wa kijamii, kuanzisha uhuru wa kiuchumi kwa
Wacuba na pia mgawanyo ulio sawa wa utajiri wa taifa hilo kupitia uongozi
uliobora wa serikali ambao utasimamia vema mali na uchumi wa taifa.
Hotuba zake, mchango wake kisiasa na mambo mengine mengi yalimfanya Castro kutambuliwa kama sio kuwa na nguvu katika chama. Mwaka 1947, Castro alijiunga na kundi la wanasiasa wahamiaji kutoka katika nchi za Caribbean ambalo liliweka makazi yake nchini Cuba.
Pamoja na wanasiasa hao, Castro waliingia katika mapinduzi ya kumpindua dikteta wa Jamhuri ya Dominica Rafael Trujilo, lakini kwa bahati mbaya mapinduzi hayo hayakufanikiwa baada ya mapinduzi hayo kuanzia nchini Cuba.

Katika mwezi Aprili mwaka 1948, Castro alihudhuria mkutano wa tisa
wa harakati wa umoja wa Wamarekani weusi uliofanyika mjini Bogota nchini
Columbia.
Lakini baada ya kuwasili nchi Colombia, Castro na rafiki yake Rafael Del Pino, walivuruga mkutano huo kwa kuonesha ujumbe uliokuwa katika vijitabu (makabrasha) yakiushutumu ushawishi wa nchi ya Marekani katika nchi za marekani ya kusini.
Siku chache baadae, kiongozi wa chama cha kudai uhuru cha Colombia Alfredo Gaitan akauawa kwa sababu za kisiasa, hali hii ilipelekea wanafunzi kuandamana mitaani.

Baadae Castro akalaumiwa kwa kuchochea machafuko yaliyojulikana kama
Bogotazo, lakini Castro alikuwa ni zaidi ya mtazamaji.
No comments:
Post a Comment