Thursday, February 13, 2014

WAKIMBIZI WA KIPALESTINA




Taarifa za idara ya Habari ya Kipalestina inaeleza kuwa, wakimbizi wa kipalestina wametapakaa kwa wingi kwenye nchi za jirani, ambapo idadi ya Wapalestina ilikadiriwa kufikia watu 7,766,185 kwa mwaka 1998. asilimia 54 wakiishi nje ya mipaka ya Palestina na kukusanyika kwa wingi katika maeneo mengine ya ulimwengu wa Kiarabu, huku wengi wao wakiishi katika nchi za Jordan, Syria na Lebanon. 
Kwa maneno mengine wanaishi katika maeneo ya jirani kutokana na kitendo cha kuwafukuza katika makazi yao kilichotokana na Janga la mwaka 1948 lililopelekea wengi wao kukimbilia katika nchi za Kiarabu zinazopakana na Palestina.

Jordan:
Kiwango cha wakimbizi wa kipalestina ni (31.4%) ya idadi ya watu wa Jordan na ni zaidi ya (42%) ya wakimbizi wote wa Kipalestina.
Sensa ya wakimbizi wa Kipalestina nchini Jordan inaonesha kuwepo kwa takribani wakimbizi milioni moja, asilimia 18 ya watu hao wakiishi katika makambi kumi ambayoyalihifadhi watu wapatao 280,000 kulingana na rekodi ya UNRWA.

Idadi ya wakimbizi wanaoishi nchini Jordan iliongezeka tangu lilipotokea janga hilo lililotajwa hapo juu ambapo kwa mwaka 1948 idadi yao ilikadiriwa kufikia watu 100.000. Watu hawa niwale waliovuka Mto Jordan na kuishi katika makambi mbalimbali. 
Baada ya Israeli kuyavamia na kuyakalia kimabavu maeneo ya Ukingo wa Magharibi na Ukanda waGaza katika mwaka 1967 wimbi jipya la watu waliofukuzwa katika makazi yaolilimiminika na idadi yao kufikia watu wapatao 240.000.2-

Syria:
kiwango cha wakimbizi wa Kipalestina nchini Syria ni (10.2%) ya wakimbizi wote waliosajiliwa, ambao wanawakilisha asilimia 2.3 ya wakazi wote wa Syria. Zaidi ya asilimia 30 ya wakimbizi wote wa Kipalestina nchini Syria wanaishi katika haya makambi.
Kambi ya Al-Yarmok inayohifadhi zaidi ya Wapalestina 100.000 haimo katika orodha ya makambi rasmi yaliyo chini ya UNRWA, licha ya huduma zake mbali mbali kuenea katika kambi hiyo. Wakimbizi walio nchini Syria wanatoka katika mikoa ya kaskazini mwa Palestina, hususan Safad na Haifa.

Wakimbizi hao niasilimia 62 ya wakimbizi wote. Wengine walitokea katika miji ya Yafa, Tiberias, Akkana miji mingine.

Mwaka 1967 zaidi ya watu 100,000 walihama kutoka katika Milimaya Golan (Golan Heights) wakiwemo wakimbizi wa Kipalestina. kuelekea maeneombalimbali ya Syria. Aidha, maelfu ya Walebanon walikimbilia Syria wakati wa vitavya kiraia vilivyoivuruga Lebanon mwaka 1982.3-

Lebanon:
baadhi ya wakimbizi wa Kipalestina walielekea Lebanon baada ya Janga la mwaka 1948. Wakimbizi hao ni asilimia 10 ya wakimbizi wote wa Kipalestina nawanaunda asilimia 10.5 ya watu wote wa Lebanon. Kwa sasa kuna kambi kumi na mbili za wakimbizi wa Kipalestina kwenye ardhi ya Lebanon, ambapo wakimbizi hao wanakabiliwa na matatizo mengi, matatizo muhimu yakiwa yakiwa ni:

miundombinu dhaifu ya makambi, msongamano kupita kiasi na ukosefu wa ajira.Nchini Lebanon kuna kiwango kikubwa sana cha wakimbizi wa Kipalestina wanaoishi katika umaskini wa kupindukia na wamesajiliwa katika programu ya kuwa katika dhiki.
Add caption

Vilevile, wakimbizi waliopo Lebanon wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa haki za kijamii na za kiraia sambamba na ukosefu wa huduma za shirika la misaada

katika maeneo elimu, afya na huduma za kijamii. Aidha, katika kipindi cha miaka iliyofuatia vita vya kiraia, shirika la umoja wa mataifa la misaada na ustawi kwa Wapalestina (UNRWA) lilisitisha kabisa kutoa dhamana ya elimu ya bure, jambo lililopelekea kuzuka kwa matatizo kadhaa wa kadhaa,  

kama vile watu kukosa masomo, kukua kwa kiwango cha wasiojua kusoma na kuandika kilichofikia asilimia48 ya wakazi wa makambini kulingana na takwimu za hivi karibuni, ambapo idadi yawahitimu wa chuo kikuu ilididimia na kufikia asilimia 4.2.

Katika kuhitimisha mjadala wa tatizo la wakimbizi wa Kipalestina tutatoa baadhi ya maelezo yaliyotolewa katika ramani ya kanda ya shughuli na operesheni za shirika laUNRWA.
Maelezo na ufafanuzi huo unashughulikia utawanyikaji na ueneaji wa wakimbiziwaliosajiliwa na shirika hili kuanzia tarehe 30 Juni 2001.

Eneo Walio kambini Walio nje ya kambi Jumla Jordan 287.951 1.351.767 1.639.718 Lebanon  214.728 168.245 382.973 Syria 109.466 282.185 391.651 Ukingo wa Magharibi 163.139 444.631 607.770Ukanda waGaza460.031 392.595 852.626

Jumla yaMaeneo 1.235.315 2.639.423 3.874.738 Jeduali hili linatoa ushahidi wa jinsi wakimbizi hawa walivyotawanyika sehemu mbalimbali baada ya kufukuzwa katika ardhi ambayo hapo awali ilikuwa imewakusanya pamoja, yaani Palestina.

Aidha, linaonyesha kwamba wakimbizi walio nje ya kambi ni mara mbili ya wale walio ndani ya kambi, hii ikiwa na maana kuwepo kwa mateso na shida za hali ya maisha Vitendo vya kigaidi vya Wazayuni havikuanza leo bali vilikuwepo tangu siku ambayo Uzayuni uliingia kwa mara ya kwanza katika eneo la Mashariki ya Kati.   


na ushahidi mkubwawa hilo ni mauaji  ya kinyama na umwagaji damu uliofanywa na unaoendelea kufanywa na Wazayuni dhidi ya wamiliki halali wa ardhi kwa lengo la kuwalazimisha kuzikimbia ardhi zao na kuwaachia wageni wapya wa Kiyahudi.
 Vyanzo vilivyotumiwa na Kituo cha habari cha Kipalestina (Palestinian NationalInformation Center) katika kutoa uthibitisho wa Historia ya Palestina:

1 comment:

  1. JackpotCity Casino | Live | Casino site
    JackpotCity Casino is a new casino located in luckyclub.live the UK. With over 700 games to choose from, you'll have access to a wide range of welcome bonuses and more

    ReplyDelete