Thursday, February 13, 2014

SADDAM HUSSEIN ABD AL MAJID AL TIKRIT


.


Saddam Hussein Abd al-Majid al-Tikriti (28 Aprili 1937 - 30 Desemba 2006) alikuwa Rais wa Iraki, kunzia tar. 16 Julai ya mwaka wa 1979 hadi mwaka wa 2003, pia waziri mkuu wa Iraki kati ya 1994 na 2003.

Alipanda ngazi ndani ya serikali na chama cha Baath kama makamu wa rais aliyemtangulia Ahmad Hasan al-Bakr. Baada ya kupewa cheo cha rais aliua wapinzani wengi na kuimarisha utawala wake.  Akaanzisha vita mbili:
  • Vita kati ya Irak na Uajemi                                                (1980 - 1988) aliyoanzisha baada ya kuona jeshi la Uajemi lilidhoofishwa kutokana na mapinduzi ya Ayatollah Khomeini; alishindwa kufikia shabaha zake akalazi mishwa kukubali mkataba wa kusalimu amri na Uajemi.
  •  
  • Vita ya Ghuba ya 1990/91                                        alipoamuru jeshi la Iraki kuvamia nchi jirani ya Kuweit; hatua hii ilijibiwa na amri ya Umoja wa Mataifa Wairaki waondoe tena walipokataa jeshi la kimataifa lililoongozwa na Marekani lilifukuza Wairaki atika Kuweit 

Ndani ya Iraki alipigania upinzani wa sehemu kubwa za wananchi hasa katika kempeni dhidi ya Wakurdi katika kaskazini ya Iraki wakati wa vita dhidi ya Uajemi na dhidi Washia wa Iraki Kusini baada ya vita ya ghuba.

Saddam Hussein aliondolewa madarakani wakati wa uvamizi wa Iraki na Marekani katika vita ya pili ya ghuba mwaka 2003. Alienda mafichoni kwa miezi kadhaa akakamatwa na kupelekwa mbele ya mahakama ya Kiiraki iliyompa hukumu ya mauti kwa jina dhidi ya binadamu na hasa kesi 148 za mauaji zilizothibitishwa mahakamani. Alinyongwa Desemba 2006 katika kambi la kijeshi mjini Al Kadhimiya nchini Iraki


No comments:

Post a Comment