Makamu wa rais wa Sudan, John Garang
ameaga dunia katika ajali ya helikopta. Garang alikuwa akirudi Sudan kutoka
Uganda ambako alikutana na rais Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Sudan Omar al-Bashir
amesoma taarifa katika runinga ya kitaifa akithibitisha kifo cha Garang hii
leo.
Maofisa wa Uganda wamenukuliwa na
vyombo vya habari wakisema kwamba abiria wote 14 waliokuwa wakisafiri katika
helikopta hiyo wamefariki dunia, wakati ilipoanguka karibu na mpaka wa Uganda
na Kenya.
Kufikia sasa kilichoisababisha ajali hiyo bado hakijajulikana, lakini
maofisa wanasema huenda ilisababishwa na hali mbaya ya hewa.
Kwa miongo miwili Garang, mwenye
umri wa miaka 60, aliongoza upinzani dhidi ya serikali ya Khartoum akiwa katika
eneo la kusini la nchi hiyo. Mwezi Januari mwaka huu, pande hizo mbili
ziliyafikia makubaliano ya amani na Garang akawa makamu wa kwanza wa rais
yapata majuma matatu yaliyopita.
Garang na rais Bashir walitarajiwa kuunda
serikali mpya wiki hii.
John Garang, aliyekuwa Rais wa kwanza wa Sudan
Kusini kabla ya uhuru na Makamu wa kwanza wa Rais wa Sudan,
baada ya kuongoza
wanamgambo wa Sudan ya Kusini kupigania uhuru wa majimbo ya
kusini.
Sudan Kusini (Jamhuri ya Sudan Kusini, kwa Kiingereza Republic of South Sudan) ni nchi huru iliyojitenga rasmi na Sudan tarehe 9 Julai 2011, ikiwa ni ya 54 katika bara la Afrika na ya 193 duniani.
Hatua hiyo ilitokana na kwamba mwezi wa Januari 2011 wakazi wa Sudan Kusini walipiga kura juu ya swali la kujitenga na Sudan wakaamua karibu kwa kauli moja kuwa nchi huru.
Tofauti kubwa kati ya pande hizo ilikuwa kwamba katika Sudan yenyewe idadi kubwa ya watu wamekuwa Waislamu na utamaduni wao una mchaganyiko wa tabia za Kiarabu na Kiafrika pamoja na usambazaji mkubwa wa lugha ya Kiarabu. Kumbe kusini kuna Waislamu wachache, wengi ni wafuasi wa dini za jadi au ni Wakristo. Kiuchumi na kielimu kusini iko nyuma sana kulingana na kaskazini.
Nchi ina muundo wa shirikisho.
Mji mkuu ni Juba, wenye wakazi 1.118.233.
Imepakana na Sudan kaskazini, Ethiopia mashariki, Kenya, Uganda, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kusini, na Jamhuri ya Afrika ya Kati upande wa magharibi.
Inakadiriwa kwamba Sudan Kusini ina wakazi zaidi ya milioni 15, lakini kutokana na ukosefu wa sensa kwa miongo kadhaa, makisio haya yaweza kuwa si sahihi, na kuweza kuongezeka hadi karibu milioni 17.
Uchumi unategemea kilimo vijijini na cha kujikimu, lakini mwanzoni mwa mwaka 2005, uchumi alianza mpito wa kutoka vijijini na mijini katika Sudan Kusini kumeonekana maendeleo kupindukia.
Historia
Kuna nyaraka chache sana za historia ya mikoa ya kusini mpaka mwanzo wa utawala wa Misri upande wa kaskazini mapema 1820 na baadaye kuendelezwa kwa biashara ya utumwa kuingia kusini.Kabla ya wakati huo, habari zote zinapatikana kwa misingi ya historia simulizi. Kulingana na mila hizo, watu wa Niloti (Wadinka, Nuer, Shilluk) na wengine waliingia kusini mwa Sudan kwa mara ya kwanza wakati fulani kabla ya karne ya 10.
Katika kipindi cha kati ya karne ya 15 na karne ya 19, uhamiaji wa makabila, hasa kutoka eneo la Bahr al Ghazal, ulileta watu hawa katika maeneo yao ya sasa. Makabila yasiyo Niloti yaani Waazande, ambao waliingia Sudan Kusini katika karne ya 16, waliunda jimbo kubwa zaidi katika kanda hii.
Katika karne ya 18, watu wa Avungara waliingia na kwa haraka wakaweka mamlaka yao juu ya Waazande. Utawala wa Avungara ulikaa kwa muda bila kupingwa mpaka kuwasili kwa Waingereza mwishoni mwa karne ya 19.
Vizuizi vya kijiografia viliwalinda watu wa kusini kutokana na kuenea kwa Uislamu, na kuwawezesha kurejesha turathi zao za kijamii na kitamaduni na urithi wao wa kisiasa na taasisi za kidini.
Misri, chini ya utawala wa Khedive Ismail Pasha, ilijaribu kwa mara ya kwanza kuikoloni kanda hiyo katika miaka ya 1870,
na kuanzisha jimbo la Equatoria katika sehemu ya kusini. Gavana wa kwanza wa Misri alikuwa Samwel Baker, aliyeanza kuhudumu mwaka 1869, akifuatiwa na Charles George Gordon mwaka 1874 na Emin Pasha mnamo 1878.
Maasi ya Mahdist ya miaka ya 1880 yaliuyumbisha mkoa huu mchanga, na Equatoria ilikoma kuwepo kama milki ya Misri mwaka 1889. Makazi muhimu katika Equatoria yalikuwa pamoja na Lado, Gondokoro, Dufile na Wadelai.
Sudan Kusini ilitawaliwa kama eneo la pekee wakati wa ukoloni wa Kiingereza hadi 1947 ilipounganishwa na kaskazini kama nchi moja bila kuwauliza wenyeji.
Wakati wa uhuru wa Sudan mwaka 1956 viongozi wa kusini walidai haki ya kujitawala ndani ya taifa jipya, lakini mapatano yalishindikana na hali hiyo ilisababishwa kutokea kwa vita ya Anyanya kati ya 1956 na 1972.
Baada ya kipindi cha amani, vita vilianza upya mwaka 1983 wakati kanali John Garang alipounda SPLA dhidi ya badiliko la Sudan kutangazwa nchi ya Kiislamu.
Vita hivyo vya pili vilikwisha mwaka 2005 kwa mkataba wa amani ulioacha kusini kama sehemu ya kujitawala ndani ya Sudan hadi ipigwe kura juu ya swali la kujitenga iliyopangwa kwa mwaka 2011.
Nchi imeathiriwa vibaya na vita vya kwanza vya Anya-nya (1) na vya pili Anya (2) na pia Vita vya Pili vya Wenyewe kwa Wenyewe vya Sudan vya SPLA / M kwa karibu miaka 21 tangu historia ya mwanzo wa SPLA / M mwaka wa 1983 - na kupelekea
kutelekezwa vibaya, ukosefu wa miundomsingi ya maendeleo, na uharibifu mkubwa na kuhama kutoka makazi yao.
Zaidi ya watu milioni 2.5 wameuawa, zaidi ya milioni 5 kuachwa bila makao na wengine kuwa wahamiaji wa ndani, na kuwa wakimbizi kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na sababu zingine zinazohusiana na vita.
Baada ya kifo cha John Garang, majeshi ya Southern Sudan Army na South Sudan Defense Force (SSDF) yalisitisha uhasama wao na kuungana mnamo Januari 2006, chini ya Azimio la Juba. SSDF ilianzishwa na Makamu wa Rais wa sasa wa Sudan Kusini, Dkt.
Riek Machar. Chini ya Azimio la Juba, Jenerali Matip akawa Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Sudan Kusini, na vikosi vyake vya SSDF kuingizwa katika Jeshi la Sudan Kusini, na kuongezea safu yake kutoka 50,000 hadi 309,000. Jumla ikawa askari 359,000.
Wote sasa ni jeshi moja linalojulikana kama Jeshi la Sudan Kusini. Jenerali Oyay Deng Ajak aliteuliwa kuwa Ofisa-mkuu-wa-Watumishi wa Jeshi la Sudan Kusini, hadi Mei 2009 wakati alipompisha Meja Jenerali James Hoth Mai
Mbali na Katiba ya Mpito ya Jamhuri ya Sudan , Katiba ya Mpito ya Sudan Kusini ya 2005 iliwekwa kuwa sheria kuu ya Sudan Kusini.
Katiba imeweka Tawi Kuu linaloongozwa na Rais ambaye ni Mkuu wa Nchi, Mkuu wa Serikali, na Kamanda Mkuu wa Sudan People's Liberation Army. John Garang, mwanzilishi wa SPLA / M alikuwa Rais wa kwanza hadi kifo chake tarehe 30 Julai 2005.
Salva Kiir Mayardit, naibu wake, aliapishwa kama Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudan na Rais wa Serikali ya Sudan Kusini tarehe 11 Agosti 2005. Riek Machar aliingia mahala pake kama Makamu wa Rais.
Nguvu za kuunda sheria ziko mikononi mwa serikali na Bunge la pamoja la Sudan Kusini.
Katiba pia imeweka mahakama huru, chombo cha juu kabisa kikiwa Mahakama Kuu.
Idadi ya Watu
Inakubaliwa na wengi kuwa kabila kubwa zaidi Sudan Kusini ni Dinka, ikifuatiwa na Nuer kisha Shilluk. Makabila mengine ya jamii ya Sudan Kusini ni Acholi, Murle, Bari, Nubi, Kuku, Funj, Maban, Zandi, Oduk na mengineyo.Sensa ya Tano ya Watu na Makazi ya Sudan (2008)
"Sensa ya Tano ya Watu na Makazi ya Sudan" nzima, ilifanywa mwezi Aprili 2008. Hata hivyo matokeo ya sensa ya Sudan Kusini yalikataliwa na viongozi wa Sudan ya Kusini kwa makisio kuwa "Ofisi kuu ya Takwimu mjini Khartoum ilikataa kutoa takwimu za kitaifa za sensa ya Sudan kwa kituo cha Sudan kusini cha Sensa, takwimu na tathmini." [8] Sensa ya Sudan Kusini ilionyesha kuwa idadi ya watu ilikuwa million 8.26[2], [9] hata hivyo Rais Salva Kiir "alishuku kuwa takwimu zilikuwa zinapunguzwa katika baadhi ya maeneo na kuongezwa katika mengine, na hivyo kufanya Hesabu ya mwisho "kutokubalika"." [10] Alidai pia kuwa idadi ya watu wa Sudan Kusini ilikuwa thuluthi moja ya tatu wa Sudan, ilhali sensa ilionyesha kuwa ni asilimia 22 pekee[9]. Ilisemekana pia kuwa watu wengi wa Sudan Kusini hawakuhesabiwa "kutokana na hali ya hewa mbaya, hali mbaya ya mitandao ya mawasiliano na usafirishaji, na baadhi ya maeneo yalikuwa hayafikiki, na watu wengi kutoka Sudan Kusini walikuwa uhamishoni katika nchi jirani na kupelekea 'matokeo yasiyokubalika', kulingana [na] mamlaka ya Sudan Kusini[10]. Mshauri Mkuu wa kiufundi wa Marekani wa sensa ya Kusini pia alisema wasajili wa sensa pengine walifikia asilimia 89 pekee ya wakazi[11].Sensa mpya
Mwaka 2009 Sudan ilianza upya sensa ya Sudan Kusini kabla ya kura ya maoni ya uhuru wa Sudan Kusini, 2011, ambayo ilisemekana pia kujumuisha Wanasudan Kusini walio nchi zingine. Hata hivyo harakati hii ilikashifiwa kwani iliziacha nje nchi zenye idadi kubwa ya watu kutoka Sudan Kusini, na badala yake kuhesabu nchi ambapo idadi hii ilikuwa ndogo[12].Lugha
Sudan Kusini inajumuisha zaidi ya makabila 200 yakizungumza lugha zinazopatikana hasa katika Sudan ya Kusini na lugha nyingine kutoka nchi jirani za Kenya, Ethiopia, Uganda, Kongo, Sudan (Khartoum) na nyingine. Lugha rasmi ni Kiingereza na Juba-Kiarabu, pamoja na lugha mbalimbali za mitaa katika majimbo au miji.Lugha tatu kubwa za Kiafrika zinazotumiwa Sudan Kusini ni Thongjieng (wazungumzaji 3,000,000 ), Thok Naadh (wazungumzaji 1,599,000), na Shilluk (zaidi ya wazungumzaji 1,000,000). Nuer inazunguzmwa katika Bentiu, Nasir, Akobo, Maywuut nk na Shilluk inazunguzmwa katika Upper Nile au katika Ufalme wa Shilluk; Juba Kiarabu inazunguzmwa karibu katika kila sehemu ya Sudan Kusini lakini hasa katika majimbo ya Equatora Mashariki, Equatoria Magharibi na Bahr el Jabel. Lugha za Wanubi zinazungumzwa sana katika milima ya Jimbo la Nuba. Lugha ya Uduk huzungumzwa na watu wa Uduk, na pia baadhi ya majirani zao. Kuna zaidi ya lugha 200 zinazozungumzwa Sudan Kusini kwa jumla, lakini kwa sasa Kiingereza ndio lugha rasmi ya Sudan Kusini.
Kima cha uwezo wa kusoma katika Sudan Kusini mwaka 2006 kilikuwa kinakadiriwa kufikia asilimia 37 kwa wanaume, 12 kwa wanawake au 24 kwa jumla kama wastani[3].
Dini
Watu wa Sudan kusini hujihusisha na imani za kitamaduni na Ukristo. Ukristo una wafuasi takriban asilimia 50 ya dini za Sudan Kusini, wengi wakiwa wa Kanisa Katoliki na Anglikana, yakiwemo pia madhehebu mengine madogo[13].Uchumi
Sehemu kubwa ya bajeti ya Serikali ya Sudan inatoka kwa pesa za mafuta. Mafuta na rasilimali nyingine za madini za Sudan Kusini zinaweza kupatikana karibu kila mahali, lakini Bentiu inajulikana kama jimbo lenye utajiri wa mafuta.Mafuta
Katika miaka ya hivi karibuni, uchimbaji wa kiasi muhimu na makampuni ya kigeni umeanza huko Sudan Kusini, na kuinua hadhi yake ya kijiografia na ya kisiasa. Khartoum imegawanya Sudan katika vitalu, na takriban asilimia 85 ya mafuta hutoka Kusini.Vitalu 1, 2, na 4 hudhibitiwa na kampuni kubwa zaidi kutoka ng'ambo, inayoitwa Greater Nile Petroleum Operating Company (GNPOC). GNPOC inajumuisha washiriki wafuatao: CNPC (Jamhuri ya Watu ya China), na hisa asilimia 40; Petronas (Malaysia), na asilimia 30; ONGC (India), na asilimia 25; na Sudapet ya serikali kuu ya Sudan na asilimia 5[onesha uthibitisho].
Vitalu vingine vinavyotoa mafuta katika Kusini ni vitalu 3 na 7 katika Upper Nile ya Mashariki. Hivi vinadhibitiwa na Petrodar ambayo inamilikiwa kwa asilimia 41 na CNPC ya China, asilimia 40 na Petronas, asilimia 8 na Sudapet, asilimia 5 na Gulf Petroleum na asilimia 5 na Al Thani.[onesha uthibitisho]
Kitalu kingine muhimu cha Kusini, kiitwacho Kitalu B na Khartoum, kinadaiwa na wadau kadhaa. [[Total/0} ya Ufaransa ilipatiwa kandarasi ya kitalu hicho chenye kilomita mraba 90,000 katika miaka ya themanini lakini tangu wakati huo imefanya kazi chache huku ikidai "force majeure"|Total/0} ya Ufaransa ilipatiwa kandarasi ya kitalu hicho chenye kilomita mraba 90,000 katika miaka ya themanini lakini tangu wakati huo imefanya kazi chache huku ikidai "force majeure"]]. Vipengele mbalimbali vya SPLM vilitoa kitalu hiki au sehemu zake kwa wadau wengine wa Sudan Kusini. Mikataba kadhaa kama hii aliyofanywa kabla ya Naivasha ilidhalilishwa wakati kiongozi wa SPLM / A Dkt John Garang de Mabior alipoondoka mamlakani. Kampuni moja katika Sudan Kusini, inadai kwamba Serikali ya Sudan Kusini imekubali mikataba yake ya kabla ya CPA[onesha uthibitisho]. Kandarasi hizi zilikuwa zimeungwa mkono na marehemu Dkt John Garang na kukabidhiwa kwa serikali ya Sudan Kusini, ambayo awali ilitia saini makubaliano mnamo Septemba 2005 kama kiongozi wa SPLM / A na imeunga mkono hadharani mikataba inayosimamiwa na Sudan Kusini[onesha uthibitisho]
Sehemu ya CPA kuhusu ugavi wa mali inasema kwamba mikataba yote iliyotiwa saini kabla ya CPA itasalia; haitakuwa kuangaliwa upya na Tume ya Kitaifa ya Mafuta (NPC), tume iliyoanzishwa na CPA na inayojumuisha Khartoum na wawakilishi wa kusini na uenyekiti wa ushirikiano baina ya Rais Al-Bashir wa Khartoum na Rais Kiir wa Sudan Kusini. Hata hivyo, CPA haielezi bayana ni nani ana uwezo wa kutia saini mikataba ya kabla ya CPA. Pande zote mbili za Khartoum na Sudan Kusini zimewahi kujaribu kudai uwezo wa kutia saini makubaliano chini ya haki ya "self determination" iliyopewa upande wa kusini[onesha uthibitisho] ambayo ilitangaza mnamo 19 Septemba 2009 katika nchi zaidi ya 105 duniani kote.
Hali ya kibinadamu
Sudan Kusini ilikiri kuwa na baadhi ya viashiria vya afya vibaya zaidi duniani[14]. [15] Mwaka 2004, kulikuwa na madaktari wapasuaji watatu tu kutumikia Sudan kusini yote, na hospitali sawa tatu, na katika baadhi ya maeneo hayo kuna daktari mmoja tu kwa kila watu 500,000[14].Kufikia wakati wa Mkataba Mwafaka wa Amani wa 2005, mahitaji ya kiutu katika Sudan Kusini yalikuwa makubwa. Hata hivyo, mashirika ya kibinadamu chini ya uongozi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) yaliweza kuhakikisha kuna fedha za kutosha kuleta unafuu kwa wakazi. Pamoja na misaada ya dharura na maendeleo, miradi ya kibinadamu ilijumuishwa katika Mpango wa Kazi wa 2007 wa Umoja wa Mataifa na washirika wake.
Mnamo 2007, OCHA (chini ya uongozi wa Eliane Duthoit) ilianza awamu ya kumalizia Kusini mwa Sudan mahitaji ya kibinadamu polepole lakini kwa kugeuka juu ya udhibiti wa kufufua na maendeleo ya shughuli za NGOs na mashirika ya kijamii. [16]
No comments:
Post a Comment