Mahakama inayoungwa
mkono na Umoja wa Mataifa imempata na hatia aliyekua Rais wa Liberia, Charles
Taylor, kwa kosa la kushiriki na kusaidia uhalifu dhidi ya binadamu, mauaji,
ubakaji na ugaidi.
Mahakama ya huko The
Hague imesema kua Bw Taylor anawajibika kwa kuunga mkono waasi wa kundi
lililojulikana kama RUF yaani Revolutionary United Front katika nchi jirani ya
Sierra Leone wakati wa vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe katika miaka 1990.
Bw Taylor ndiye
kiongozi wa kwanza kutoka Afrika kukabiliwa na hukumu mbele ya Mahakama ya
Kimataifa tangu kesi maarufu za Nuremburg baada ya vita vikuu vya pili vya
Dunia. Atahukumiwa mwezi ujao.
Maelezo yafuatayo
yalikusanywa na kuandikwa na mwandishi wa BBC aliye nchini Liberia na mara
kadhaa alikutana na Charles Taylor.
Charles Taylor alikua
Rais wa Liberia kuanzia mwaka 1997 hadi alipojiuzulu mnamo mwaka 2003 kufuatia
shinikizo kali za kimataifa. Alianza shughuli za siasa wakati wa ziara yake
nchini Liberia kama kiongozi wa msafara wa mashirika ya Waliberia yaliyo barani
Amerika mapema katika muongo wa 1980, mapinduzi ya kijeshi yalipofanyika naye
kupewa kazi katika serikali ya Samuel Doe.
Baada ya kuteuliwa
kama Naibu waziri katika Wizara ya biashara ya serikali ya Rais Doe, Taylor
aliikimbilia Marekani kufuatia madai kwamba amepoteza takriban dola za
kimarekani milioni moja.
Alifungwa huko
Marekani lakini akatoroka jela katika mazingira ambayo hadi leo bado ni ya
kutatanisha. Hatimaye aliunda kundi lake la waasi, lililojulikana kama National
Patriotic Front of Liberia, ambalo liliiondoa serikali ya Samuel Doe
madarakani.
Alikuwa kiongozi wa
waasi
Taylor ana kipaji cha
kua mtu mchangamfu ambaye aliweza kumbadili adui na kumpenda kiasi cha kumfanya
kua mfuasi sugu. Kwa mfano alipoingia mji wa Monrovia mnamo mwaka 1995 makumi
kwa mamia ya watu waliompinga walijitokeza kumpokea na kumuimbia nyimbo za
kumsifu kama shujaa.
Licha ya kuwateua watu
wengi kama washauri wake lakini hiyo ilikua danganya toto'' kwa sababu
hakufuata ushauri wao hata siku moja. Mmoja wa washauri wake wa karibu aliwahi
kuniambia kua yaliyomfika Taylor yangeweza kuepukika kama angewasikiliza
washauri hao.
Taylor alipenda sana
kujifananisha na watawala wa enzi ya karne ya kumi na tisa kwa jinsi
alivyowazawadia fukara akifahamu kua fadhila zake zitamjengea sifa na kumfaa
siku moja.
Akiwa mpenda madaha
alifahami vyema nguvu ya vyombo vya habari na jinsi ya kuvitumilia. Kupitia
miaka ya 1990 alishiriki mahijiano mengi ya kipindi cha BBC cha Focus on
Africa.
Katika kipindi cha
kwanza, akiwa ni kiongozi wa kundi la waasi asiyefahamika, alitangaza mpango
wake wa kuivamia Liberia.
Miaka michache
baadaye, alipodokezewa na mtangazaji kwamba watu wengi wanamuonelea kua
muuwaji, alilipuka na kusema ''Hata Yesu Kristu alituhumiwa kua ni muuwaji enzi
zake.
Katika mahojiano mengi
tuliyofanya naye daima alijitahidi kudhibiti mahojiano ili kutoa sura
inayompendeza yeye. Mfano uilipomrushia suali lililomchukiza alijitahidi
kulibadili liweze kusikika kwa manufaa yake.
Kama mpiganaji mahiri
alijivunia uwezo wake wa kiume na uwezo wa kuzaa watoto wengi. Hakuficha siri
yake ya kupenda wanawake, akidokeza wakati mmoja kua kama kiongozi wa Kiafrika
ana haki ya hadi wake wanne.
Mwanamitindo Naomi
Campbell alihusishwa katika kesi ya Taylor
Wakosoaji wake
walipokashifu tabia yake ya uzinzi, alijibu kwa kuwakemea wanaume wanaofanya
mapenzi ya jinsia moja na kujibu ''Bora mimi nawapenda wanawake.''
Mnamo mwaka 1996
alidokezea kua angetaka kujaliwa na watoto wengine watano na wote watakua
wanaume. Hata hivyo hakujaliwa na ndoto yake hio watoto wake wawili waliofuata
walikua wa kike.
Labda kama ishara ya
kujiliwaza majaliwa hayo, aliwahi kuniambia kua kama mzazi anayewapenda wanawe,
mume yeyote atakayewaoa wanangu, itabidi akubali watoto wake warithi jina la
Taylor liendelee kudumu katika familia yao.
CHANZO: bbc Swahili
No comments:
Post a Comment