Patrice Lumumba baba wa taifa la Congo
RAIS JOSEFU KABILA NA MKEWE |
Nchi kubwa na yenye rasilimali nyingi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo (DRC) imekuwa katika kile kinachotajwa kuwa vita vya Dunia vya Afrika.
Hali hiyo imeaicha nchi katika janga la kuhitaji misaada ya kibinaadamu.
Mapigano ya miaka mitano yalitikisa serikali, ikiungwa mkono na
Angola, Namibia na Zimbabwe, dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Uganda na
Rwanda.
Licha ya mpango wa amani na kuundwa kwa serikali ya mpito mwaka
2003, watu upande wa mashariki mwa nchi hiyo wamesalia kuwa katika hali ya
wasiwasi kutokana na kuwepo kwa makundi ya wanamgambo na wanajeshi
yanayowasumbua.
Vita hivyo vilisababisha vifo vya takriban watu milioni tatu, ama
kutokana na mapigano ya moja kwa moja au kutokana na magonjwa na utapia mlo.
Hali hiyo imetajwa kuwa huenda ndio baa kubwa kuwahi kutokea barani Afrika
katika miaka ya hivi karibuni.
Vita hivyo vilikuwa na athari za kiuchumi na za kisiasa. Mapigano
yalichochewa na hazina kubwa ya utajiri wa madini, huku pande zote mbili
zikitumia mwanya huo kufuja rasilimali. Historia ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya
Kongo imekuwa na sura mbili, moja ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na ya
ufisadi. Baada ya uhuru mwaka 1960, nchi hiyo mara moja ilikabiliwa na jeshi
kufanya mgomo na jaribio la kutaka kujitenga kwa jimbo lenye utajiri wa madini
la Katanga.
Mwaka mmoja baabaye, waziri mkuu wa wakati huo Patrice Lumumba
alikamatwa na kuuawa na wanajeshi wanaomtii mkuu wa majeshi Joseph Mobutu.
Mwaka 1965 Mobutu alichukua madaraka, na baadaye kuibadili jina nchi
hiyo na kuiita Zaire na yeye kujiita Mobutu Sese Seko. Aliigeuza Zaire kuwa
eneo la harakati dhidi ya Angola iliyokuwa ikiungwa mkono na Jamhuri ya
Kisovieti na hivyo yeye kupata kuungwa mkono na Marekani. Lakini pia
aliidumbukiza Zaire katika ufisadi.
Baada ya vita baridi, Zaire ilipoteza umuhimu wake kwa Marekani.
Hivyo, mwaka 1997, wakati nchi jirani ya Rwanda ilipovamia Zaire kuwasaka
wanamgambo wa Kihutu, iliwapa nafasi waasi wanaompinga Mobutu ambao mara moja
waliuteka mji wa Kinshasa na Laurent Kabila kuingia madarakani na kuwa rais na
kulirejesha jina la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Hata hivyo, matatizo ya DRC yaliendelea. Mzozo kati ya Bw Kabila na
washirika wake wa zamani ulianzisha uasi mwingine, uliokuwa ukiungwa mkono na
Rwanda na Uganda. Angola, Namibia na Zimbabwe zikachukua upande wa Kabila na
hivyo kuigeuza nchi hiyo kuwa uwanja wa vita.
Majaribio ya kupindua serikali na ghasia za hapa na pale ziliendelea
kurindima na kuanzisha mapigano mapya mashariki mwa nchi hiyo mwaka 2008.
Wanamgambo wa Kihutu kutoka Rwanda walipambana na wanajeshi wa serikali mwezi
Aprili na kusababisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao.
Kundi jingine la waasi chini ya Jenerali Laurent Nkunda lilitia
saini makubaliano ya amani mwezi Januari, lakini mapigano yalizuka tena mwezi
Agosti. Majeshi ya Jenerali Nkunda yalisonga mbele na kuingia katika ngome za
serikali na mji wa GOma na kusababisha raia na wanajeshi kukimbia huku majeshi
ya kulinda usalama ya Umoja wa Mataifa kujaribu kushikilia maeneo pamoja na
wanajeshi waliosalia wa serikali.
Katika jaribio la kuleta hali ya utulivu, serikali mwezi Januari
mwaka 2009 ilialika wanajeshi kutoka Rwanda kusaidia kuwasaka waasi wa Kihutu
wanaofanya shughuli zao mashariki mwa DRC.
Rwanda ilimkamata hasimu mkuu wa waasi wa Kihutu, Jenerali Nkunda,
ambaye ni Mtutsi aliyeonekana kama mpinzani mkuu katika eneo hilo.
Hata hivyo, mwaka 2009, ulisalia kuwa na hali ya wasiwasi katika
maeneo ya mashariki.
Historia fupi ya DRC
Nchi kubwa
na yenye rasilimali nyingi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) imekuwa
katika kile kinachotajwa kuwa vita vya Dunia vya Afrika. Hali hiyo imeaicha
nchi katika janga la kuhitaji misaada ya kibinaadamu.
Mapigano ya miaka mitano yalitikisa serikali, ikiungwa mkono na Angola, Namibia na Zimbabwe, dhidi ya waasi wanaoungwa mkono na Uganda na Rwanda.
Licha ya mpango wa amani na kuundwa kwa serikali ya mpito mwaka 2003, watu upande wa mashariki mwa nchi hiyo wamesalia kuwa katika hali ya wasiwasi kutokana na kuwepo kwa makundi ya wanamgambo na wanajeshi yanayowasumbua.
Vita hivyo vilisababisha vifo vya takriban watu milioni tatu, ama kutokana na mapigano ya moja kwa moja au kutokana na magonjwa na utapia mlo. Hali hiyo imetajwa kuwa huenda ndio baa kubwa kuwahi kutokea barani Afrika katika miaka ya hivi karibuni.
Vita hivyo vilikuwa na athari za kiuchumi na za kisiasa. Mapigano yalichochewa na hazina kubwa ya utajiri wa madini, huku pande zote mbili zikitumia mwanya huo kufuja rasilimali. Historia ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imekuwa na sura mbili, moja ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na ya ufisadi. Baada ya uhuru mwaka 1960, nchi hiyo mara moja ilikabiliwa na jeshi kufanya mgomo na jaribio la kutaka kujitenga kwa jimbo lenye utajiri wa madini la Katanga.
Mwaka mmoja baabaye, waziri mkuu wa wakati huo Patrice Lumumba alikamatwa na kuuawa na wanajeshi wanaomtii mkuu wa majeshi Joseph Mobutu.
Mwaka 1965 Mobutu alichukua madaraka, na baadaye kuibadili jina nchi hiyo na kuiita Zaire na yeye kujiita Mobutu Sese Seko. Aliigeuza Zaire kuwa eneo la harakati dhidi ya Angola iliyokuwa ikiungwa mkono na Jamhuri ya Kisovieti na hivyo yeye kupata kuungwa mkono na Marekani. Lakini pia aliidumbukiza Zaire katika ufisadi.
Baada ya vita baridi, Zaire ilipoteza umuhimu wake kwa Marekani. Hivyo, mwaka 1997, wakati nchi jirani ya Rwanda ilipovamia Zaire kuwasaka wanamgambo wa Kihutu, iliwapa nafasi waasi wanaompinga Mobutu ambao mara moja waliuteka mji wa Kinshasa na Laurent Kabila kuingia madarakani na kuwa rais na kulirejesha jina la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Hata hivyo, matatizo ya DRC yaliendelea. Mzozo kati ya Bw Kabila na washirika wake wa zamani ulianzisha uasi mwingine, uliokuwa ukiungwa mkono na Rwanda na Uganda. Angola, Namibia na Zimbabwe zikachukua upande wa Kabila na hivyo kuigeuza nchi hiyo kuwa uwanja wa vita.
Majaribio ya kupindua serikali na ghasia za hapa na pale ziliendelea kurindima na kuanzisha mapigano mapya mashariki mwa nchi hiyo mwaka 2008. Wanamgambo wa Kihutu kutoka Rwanda walipambana na wanajeshi wa serikali mwezi Aprili na kusababisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao.
Kundi jingine la waasi chini ya Jenerali Laurent Nkunda lilitia saini makubaliano ya amani mwezi Januari, lakini mapigano yalizuka tena mwezi Agosti. Majeshi ya Jenerali Nkunda yalisonga mbele na kuingia katika ngome za serikali na mji wa GOma na kusababisha raia na wanajeshi kukimbia huku majeshi ya kulinda usalama ya Umoja wa Mataifa kujaribu kushikilia maeneo pamoja na wanajeshi waliosalia wa serikali.
Katika jaribio la kuleta hali ya utulivu, serikali mwezi Januari mwaka 2009 ilialika wanajeshi kutoka Rwanda kusaidia kuwasaka waasi wa Kihutu wanaofanya shughuli zao mashariki mwa DRC.
Rwanda ilimkamata hasimu mkuu wa waasi wa Kihutu, Jenerali Nkunda, ambaye ni Mtutsi aliyeonekana kama mpinzani mkuu katika eneo hilo.
Hata hivyo, mwaka 2009, ulisalia kuwa na hali ya wasiwasi katika maeneo ya mashariki.

"Ni kijana na anawakilisha mustakabali wa nchi," Ndivyo
walivyosema wafuasi wa Joseph Kabila wakati akiwasilisha fomu ya kugombea urais
kwa muhula wa pili mwezi Septemba.
Akiwa na
miaka 40, rais huyo anayetetea kiti chake ndio mgombea mwenye umri mdogo zaidi,
ingawa tayari amekaa madarakani kwa miaka 10.
Alikuwa kamanda aiye na makuu katika jeshi, wakati baba yake Laurent-Desire Kabila alipouawa mwaka 2001, na aliteuliwa na watu wa karibu na utawala wa baba yake kuongoza DRC wakati huo ikitikiswa na mizozo mbalimbali ya wapiganaji.
Baadaye mwaka 2006 Bw Kabila alipata ushindi katika uchaguzi mkuu wa kwanza wa kidemokrasia tangu uhuru.
Rais Kabila anaungwa mkono zaidi katika eneo la mashariki ambapo ndio alikozaliwa.
Alipata uungwaji mkono kidogo sana kutoka kwa wapiga kura wa upande wa magharibi katika uchaguzi wa mwaka 2006, huku wanaharakati wengi wa upande wa upinzani wakimtuhumu, bila ushahidi wowote, kuwa ni mzaliwa wa nchi jirani ya Rwanda, nchi ambayo imeivamia mara mbili DRC.
Bw Kabila alikulia nchini Tanzania na anazungumza Kiswahili na Kiingereza vizuri zaidi kuliko lugha zinazozungumzwa zaidi mjini KInshasa, yaani Kilingala na Kifaransa, lugha ambazo alilazimika kujifunza akiwa madarakani.
Kwa muda mwingi akiwa madarakani amekuwa kimya, akivunja ukimya huo tu wakati akizindua kampeni yake ya uchaguzi kwa kufanya mkutano na waandishi wa habari kwa muda wa saa tatu.
"Hatutapoteza uchaguzi huu. Nina uhakika na watu wetu, wameshuhudia jitihada na kujitolea," alisema.
Kampeni ya Bw Kabila ina msemo usemao "Maeneo matano ya ujenzi katika jamhuri", akiwa na maana ya miradi ya ujenzi wa miundombinu ya nchi, hasa ujenzi wa barabara na vituo vya nishati.
Lakini wananchi wengi wa Kongo wanalalamika kuwa kasi ya maendeleo ya kijamii ni ndogo mno.
Rais Kabila amekiri kuwepo kwa jambo hilo, akisema ana deni la kulipa kwa wapiga kura wa DRC na anawataka wamchague tena ili apate nafasi ya kulipa deni hilo.

Vital Kamerhe, 52, aliwahi kuwa mshirika wa rais Kabila, lakini sasa
yuko upande wa upinzani.
Akiwa mmoja wa waasisi wa chama cha PPRD
cha Kabila, Bw Kamerhe aliongoza kampeni za urais mwaka 2006 za Kabila.
Baadaye alikuwa spika wa bunge, hadi alipozozana na rais kuhusiana na makubaliano ya siri na rais ya kuruhusu Rwanda kupeleka wanajeshi wake mashariki mwa nchi kuwasaka waasi mapema mwaka 2009.
Bw Kamerhe ni mzaliwa wa upande wa mashariki katika mkoa wa Kivu, na aliojitoa serikalini na kuanzisha chama chake cha UNC.
Vital Kamerhe ni mwanasiasa na msomi anayezungumza vyema Kifaransa na Kiingereza, pamoja na lugha rasmi nne za Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Anajiuza kwa wapiga kura wake -- kama mfano kwa kujifananisha na rais wa zamani wa Brazil Ignacio Lula da Silva.
"Nina uhakika kuwa eneo letu kijiografia na rasilimali, DRC kwa sasa ni kama tembo aliyelala, na ataamka kama Brazil," alisema.
Mtindo wake wa kufanya kampeni ni wa kiubunifu, akifanya mikutano katika maeneo wanaoishi watu maskini na kufanya mihadhara ya majadiliano ambapo watu wanakuwa huru kumuuliza maswali moja kwa moja.
Lakini wafuasi wengi wa upinzani bado wanamuona kama mtu aliye karibu sana na Bw Kabila, na ni mmoja wa wagombea 10 wanaotaka kuchukua kura kutoka kwa rais.
Akiwa na umri wa miaka 79, Bw Etienne Tshisekedi, ndio mgombea mwenye umri mkubwa zaidi. Alizaliwa katika mkoa wa Kasai ya Kati mwezi Disemba mwaka 1932.
Alisomea sheria wakati wa utawala wa ukoloni wa Ubelgiji. Aliingia katika siasa wakati DRC ikipata uhuru mwaka 1960, ambapo alianza kwa kupata nyadhifa mbalimbali za ngazi ya juu serikalini, na pia katika utawala uliodumu kwa muda mfupi wa Kasai.
Alikuwa waziri wakati wa utawala wa kidikteta wa Mobutu Sese Seko, na alihamia upande wa upinzani mwaka 1980 wakati Bw Mobutu alipoamua kufuta uchaguzi wote.
Akiwa kiongozi wa chama cha UDPS, Bw Tsisekedi amekuwa mpinzani wa serikali mbalimbali tangu wakati huo.
Wakati Mobutu alipolazimishwa kuipeleka serikali yake katika mfumo wa vyama vingi mapema miaka ya 1990, Bw Tshisekedi alikuwa waziri mkuu mara mbili katika kipindi cha miaka miwili.
Aliondoka madarakani mara hizo mbili kutokana na mivutano mikali na Mobutu.
Chama cha Bw Tshisekedi hakikubeba silaha wakati wa mfululizo wa vita zilizosababisha kuanguka kwa utawala wa Mobutu mwaka 1997, na hivyo kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wananchi waliokuwa wameghubikwa na miaka mingi ya vita.
Baada ya kususia uchaguzi wa mwaka 2006, ambao alidai ulivurugwa mapema, Bw Tshisekedi ameahidi kushiriki kikamilifu safari hii na kupata ushindi.
Kwa baadhi ya watu, amevuka mipaka kwa kujitangaza kuwa ni rais kabla hata ya upigaji kura.
"Wananchi wa Kongo ni watu huru nchini humu na wamenitangaza mimi kuwa rais siku nyingi zilizopita," alisema wakati akizindua kampeni yake Novemba 11.
Wakosoaji wake wanasema matamshi kama hayo yanaweza kuchochea ghasia, hasa iwapo kama atapoteza uchaguzi.
Kukosekana kwake kwa mara kwa mara nchini humo kumeleta minon'gono kuhusu afya yake.
Bw Tshisekedi anaungwa mkono kwa kiasi kikubwa katika eneo analotoka la Kasai na ia Kinshasa.
Wafuasi wake na wale wa Bw Kabila wamefarakana kwa misingi ya kikabila katika maeneo ya kusini mwa DRC, ambapo watu wengi kutoka Kasai wamehamia huko.
Chama cha UDPS kimekita mizizi yake na umaarufu upande wa kusini, lakini sio maeneo mengine nchini humo.
CHANZO: Kutoka katika vyanzo mbalimbali magazeti na mitandao

M23 WALIA NJAA HUKO UHAMISHONI UGANDA ,WAMUOMBA KABILA AWARUHUSU WAREJE MAKWAO
Hatua ya Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kukataa kusaini
mkataba wa amani na kundi la waasi la M23, imepeleka kilio kwa kundi hilo, na
sasa wanalia njaa uhamishoni nchini Uganda.
Uganda, nchi ambayo
ni msuluhishi wa mgogoro huo, imejikuta katika wakati mgumu kwani kundi la
waasi wa M23 wapatao 1,700 limekimbilia nchini humo, ilhali Uganda ikiwa na
jukumu la kusuluhisha waasi hao na Serikali ya DRC.
Msemaji wa Serikali
ya DRC, Lambert Mende, mwishoni mwa wiki ametamka kuwa Serikali yake ina
wasiwasi kuwa Uganda ina maslahi binafsi na waasi wa M23, hivyo hawako tayari
kutia saini mkataba unaosimamiwa kwa mitego.
“Uganda sasa inaonekana kuwa sehemu ya mgogoro.
Ina maslahi na M23,” alisema Mende.
Kauli
hii ya Mende imekuja siku chache baada ya DRC kukataa kutiliana saini na waasi
kwa maelezo kuwa M23 ni kundi lililotangaza kujivunja, wamekimbilia Rwanda na
Uganda, na hivyo kulipa sharti kubwa wanalolikataa.
Sharti
hilo ni kuwa mkataba uwe na kipengele kinachowazuia M23 milele kutoshika silaha
na kuanzisha mapambano, hoja inayokataliwa na waasi, huku Uganda ikizishawishi
pande mbili zitie saini mkataba hivyo hivyo ulivyo kwa maelezo kuwa yakitokea
matatizo mbele ya safari utarekebishwa tena.
Masharti
mengine wanayowapa waasi hao ni kuwa makamanda wapatao 100 waliokuwa wanaongoza
kundi la M23, wasiruhusiwe kuingia jeshini moja kwa moja, na badala yake wapewe
mafunzo ya kijeshi, huku wakiacha fursa ya kushitaki wahalifu wa kivita
watakaothibitika mbele ya safari kuwa walitenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Uganda,
ambayo sasa hivi ina mzigo mkubwa wa kulisha waasi hao waliowekwa kambini
nchini humo tangu Jumatatu (Novemba 4) kundi hilo lilipotangaza kushindwa vita
na kuweka silaha chini, inasema hali inayoiona ikiwa waasi hao
hawatahakikishiwa usalama wao, pato la fedha na kushirikishwa serikalini, kuna
wasiwasi kuwa wanaweza kurejea msituni.
“Hawa
ni binadamu. Njaa ikiwashika, usitarajie watasubiri kufa kwa njaa. Wanaweza
kurejea msituni,” alisema afisa mmoja wa Serikali ya Uganda.
Uganda
pia imetishia kwa mara nyingine mwishoni mwa wiki kuwa ikiwa suluhu
haitapatikana haraka, na DRC ikaendelea kuituhumu kuwa inashirikiana na waasi
wa M23, basi yenyewe itajitoa katika nafasi ya kuwa msuluhishi.
Kuhusiana
na tishio la Uganda kujitoa kwenye mazungumzo, Waziri Mdogo wa Mambo ya Nje wa
Uganda, Asumani Kiyingi, amesema: “Tumewasiliana na Umoja wa Mataifa kupitia
kwa Balozi wetu jijini New York, kwani tunataka kufahamu iwapo kilichoandikwa
kwenye vyombo vya habari ni cha kweli,” amesema.
“Ikiwa
Umoja wa Mataifa utathibitisha kuwa wataalamu wake wameandika taarifa hizo za
uongo [kuwa Uganda inaunga mkono M23], basi tutajitoa katika jukumu la
usuluhishi wa mgogoro wa DRC na waasi wa M23.”
M23
kwa upande wao walioanza vita Aprili 2012 wanamtuhumu Rais Joseph Kabila kuwa
wao ndiyo waliomsaidia baba yake, Laurent Kabila, kuingia madarakani na hata
makundi ya waasi yalipokuwa yanatishia kumuondoa madarakani walimtetea, lakini
alipoingia madarakani akawatekeleza.
Wataalamu
wanasema kuwa nchi za Uganda na Rwanda pamoja na kukaripiwa na jumuiya ya
kimataifa, zikaacha kukiunga mkono kikundi cha M23, hali iliyokifanya kichapwe
kama mtoto mdogo, sasa zimehamishia nguvu kwa makundi mengine ya waasi yaliyopo
kwenye misitu ya Congo.
Shutuma
kubwa zinazosukumwa kwa nchi hizi ni kuwa zimekuwa zikinunua madini na mbao
kutoka kwa waasi, hali inayoziingizia fedha nyingi za kigeni bila kujali kuwa
zinahatarisha maisha ya Wakongo wasio na hatima, taarifa ambazo Serikali ya
Uganda imeziita za ‘kipuuzi’.
Kikosi
Maalum cha Umoja wa Mataifa kinachoongozwa na Mtanzania, Brigedia Jenerali
James Mwakibolwa, kwa kuhusisha Brigedi Maalum ya SADC, kimewachakaza M23 hadi
wakasalimu amri, lakini wachambuzi wa mambo wanasema kung’olewa kwa M23 si
mwisho wa matatizo DRC.
Richard
Mugamba, Mhariri Mtendaji wa gazeti la the Citizen, ambaye amekuwa akiripoti
habari za waasi kwa kufika Goma, anasema M23 ni moja ya makundi zaidi ya 17
yaliyoko mashariki mwa Congo.
“Kila
mtu anatambua kwamba M23 kuweka silaha chini ni furaha kwa Wakongo, ila
matatizo yao yana miaka 17. Tangu 1999 wamekufa watu milioni 5. M23 wamekuwapo
kwa miezi 24, lakini mashariki mwa Congo kuna makundi kama FDRL, Mai Mai,
RCD-Goma, ADF, kuna vikundi 17 na vyote hivi viko mashariki kwenye madini, kwenye
mbao na mkaa.
“Ni
vyema kwamba M23 imeshindwa, lakini haiwezi kuwa suluhisho tangu 1996
walipommaliza Mabutu [Sese Seko Kukubanga wa Zabanga], wamekuwa wakipigana.
Kiongozi wa waasi Laurent Nkunda yuko Uganda (CNDD). Kuna nchi ambazo
zinatuhumiwa – Rwanda na Uganda zinatuhumiwa,” amesema Mugamba. Hata
kiongozi wa sasa wa M23, Kanali Sultani Makenga, amekimbilia Uganda.
“Sisi
kama Tanzania tume-play role (tumetimiza wajibu) yetu. Kuna watu wanataka haya
makundi yawepo kwa sababu wanafanya biashara. Makenga alikuwa ana-access dola
58 milioni mwaka jana, tuseme anapata dola milioni 10, lazima wote wanafanya
biashara.
“Watu
wote wanaohusika na Congo hebu wakae chini wazungumze. Mali zinauzwa nje.
Nikiwa Congo niliona vitu ambavyo nasema sawa kuna tatizo, lakini mbona kuna
mikono mingi tu. Kama hakuna amani Congo au kwa jirani yako, wewe huwezi kuwa
na amani. Angalia hali ya usalama kwa mikoa ya Kigoma na Kagera.
“Jeshi
la UN lipo Congo kwa miaka 11, watu milioni 5 wameuawa. SADC Intervention
Brigade UN waliipinga awali, lakini angalia kazi iliyofanya kwa miezi sita.
Dunia kama ingekuwa na nia ya dhati hawa waasi wote wangekuwa hawapo,”
anasema Mugamba.
Mobhare
Matinyi, mchambuzi wa masuala ya kimataifa, anasema M23 kama kikundi kimekwisha
kwa sababu makamanda wake wamejisalimisha, na kuna taarifa kuwa Waziri wa
Mashauri ya Nje wa Marekani, John Kerry, na Waziri Mkuu wa Uingereza, David
Cameron, walimpigia simu Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kumwambia asiingilie
aache hiki kipigo kiishe.
“M23
imepigika, haina uwezo wa kuibuka tena, lakini bado kuna hatari. Kwa kuwa
Uganda viongozi wake wana maslahi binafsi nchini Congo na Rwanda ina maslahi ya
kitaifa Congo, kuna uwezekano wakaanzisha insurgence groups (makundi ya waasi)
kuleta shida kwa Congo waendelee kuvuna,” Matinyi ameiambia JAMHURI.
Anasema
bado kuna makundi yanayopigana yenyewe kwa wenyewe, baadhi ya makundi hayo ni
kama FDLR, Democratic Forces for Liberation of Rwanda, mabaki ya Interahamwe na
Banyamulenge ambao bado ni tishio.
“Majeshi
yetu Tanzania kihistoria ni nchi yenye msingi wa utu, usawa na haki. Ndiyo
maana Tanzania imekuwa ikitoa majeshi yake kumtetea Mwafrika na kumtetea
binadamu. Tulipoitikia kwenda Congo ilikuwa ni kumtetea Mwafrika, hatuwezi
kukaa miaka 20, 30 watu wakiuawa sisi tunaangalia tu,” anasema.
Swali
ni je, njaa ikiendelea kuwasumbua waasi wa M23 hawatarudi msituni? Wachambuzi
wanasema mkataba wa amani unapaswa kuharakishwa.
CHANZO: GAZETI LA JAMHURI
CHANZO: GAZETI LA JAMHURI
No comments:
Post a Comment