The North Atlantic Treaty
Organisation au Mkataba- (Muungano) wa Atlantiki ya Kaskazini kwa
kifupi 'NATO',ambayo kwa jina lingine huitwa North Atlantic Alliance,
ni Muungano wa Kijeshi baina ya Serikali mbali mbali zinazopatikana upande
wa Atlantiki ya Kaskazini.Serikali hizo au wanachama hao walisaini mkataba
tarehe 4,Aprili mwaka 1949 ni miaka 4 tu ilikuwa imepita baada ya kuisha
vita vya pili vya Dunia kufuatia Mlipuko "mabomu ya
Nuclear" nchini Japan ambapo japani hawatakaa na kusahau
shambulizi hilo lililotekelezwa na Marekani.Nchi hizo zinazounda Muungano
huo zinakwenda kwa jina la NATO na makao makuu yake
ni Brussels,Ubelgiji. Mkataba huu lengo lake ni kuunda 'mfumo wa
Ulinzi wa pamoja' ambapo wanachama wake walikubaliana kuwa na ulinzi wa
pamoja ili kukabiliana na mashambulizi yoyote yale yatakayojitokeza dhidi ya
wanachama wa NATO.
Mkataba huo ulisainiwa katika mji Washington
D.C, tarehe 4-Aprili-1949 na kuridhiwa na Marekani mwezi wa Agosti.
Katibu Mkuu wa kwanza wa NATO
alijulikana kama Bwana Ismay.Na katibu Mkuu wa sasa wa NATO ni Bwana
Anders Fogh Rasmussen.
(
Wanachama wa NATO ni zaidi ya nchi
27 wakiwemo Marekani, Uingereza, Ufaransa, na German.
Sehemu ya Matumizi ya "ulinzi wa -kijeshi- duniani"
yanayotolea na majeshi ya Muungano wa Atlantiki ya Kaskazini (NATO) ni asilimi 70%.Marekani
peke yake sehemu ya matumizi ya ulinzi wa kijeshi inayotoa ni jumla ya asilimia
43% kati ya hizo 70% .Uingereza,Ufaransa,Ujerumani,na
Italia zinatoa asilimia 15%.Na wanachama wengine waliobakia wanatoa asilimia
12% za ulizni.Muungano wa Atlantiki ya Kaskazini au NATO , tangu
kuundwa kwake hadi leo hii, umeweza kufanya 'Operesheni
za uvamizi' wa mataifa mengine kama ifuatavyo :
-Operesheni ya kijeshi ya NATO na ambayo ni ya kwanza tangu kuundwa kwa NATO ni ile ya Yugoslavia
mbayo ilianza rasmi Juni mwaka 1993 hadi Oktoba mwaka 1996.Vita
hii dhidi ya Jamhuri ya Yugoslavia iliambatana na vikwazo vya kiuchumi
pamoja na vikwazo vya -ununuzi wa- silaha.Operation nyingine dhidi ya
Yugoslavia ilikuwa tarehe 24 Machi mwaka 1999 ambapo mashambulizi ya ndege
za kivita yalidumu kwa muda wa wiki 11.
-Operesheni nyingine ilifanyika nchini Afghanistan na ambayo leo hii bado
moto wake unaendelea kuwaka, operesheni hii inaonekana kuwa ngumu zaidi kuliko
Operesheni zote walizokutana nazo Wanachama wa NATO!.Operesheni hii chanzo
chake ilikuwa ni kufuatia mashambulizi ya Kigaidi ya tarehe 9-septemba
mjini Washington ambayo ndio yaliyosababisha leo hii NATO
kuwepo Afghanistan.
Nchi hii ya Afghanistan ni nchi
yenye mapango na milima mingi sana na huko ndiko Wataliban -wanaojiita
au wanaojulikana kama watu wenye imani kali -wanakoseti makambi yao ya kigaidi
! ,hali hiyo ya kijiografia ya nchi hii imewakanganya sana wanachama wa
NATO maana kama si milima,basi Operesheni hii umri wake ungelikuwa mfupi
zaidi na kuisha haraka, lakini Watalibani hawa inaonekana hawapigiki, na
ili kuwapata walipojichimbia inabidi utumie silaha kali sana na muhimu sana
kama hii aliyonayo commando huyu anayejaribu kutafuta ili kujua
wasumbufu hawa wako kona ipi !.
-Operation nyingine ni ile ya Ghuba ya Aden na
Bahari ya Hindi ambayo ilianzishwa mwaka tarehe 17-agosti-mwaka
2009 ili kuwakandamiza Maharamia wa Somalia ambao wanazinyima meli za
kibiashara uhuru wa kupita katika bahari hizo.
*Operesheni nyingine ya
nne ni mwaka 2011 nchini
Libya dhidi ya kiongozi wa kiimla Muammar Ghadafi.
Operasheni hii chanzo chake ni uasi
wa walibya ulioanza mwaka 2011 nchini Libya,ambapo wapinzania wa serikali ya Libya au wapinzani wa Muammar Ghadafi waliamua kumtolea uvivu Ghadafi
kwa kuandamana na kumtaka ajiuzuru na kuwaachia nchi yao,Hali hii ilizua vita
kati ya wapinzani na vikosi vitiifu alivyoviunda Ghadaf ili kulinda mapinduzi ya Libya. Baada ya mapigano kati ya
Majeshi ya wanamapinduzi
na majeshi ya Ghadafi kupamba moto na
raia wengi kupoteza maisha yao wakati bado walikuwa wakitaka kuishi, na
baada ya hasara kubwa ya mapigano hayo kutokea,Umoja wa Mataifa ya Balaza
la Usalama mnamo mwezi wa Machi tarehe 17 mwaka wa 2011 ukiongozwa
na kifungu cha sheria ya mwaka 1973,uliamua kutoa amri ya kusitisha
mapigano hayo na kuyataka majeshi ya Ghadafi yalinde raia wake na sio kuua raia
wake.pia Baraza lilipitisha Azimio lililopiga marufu ndege za ghadafi kuruka
juu ya anga la Libya.Azimio hilo lililenga kuwalinda raia wa Libya waliokuwa
wakisumbuliwa na kuuliwa na ndege hizo za ghadafi.
Lakini amri hii iliyotolewa na Balaza
la Usalama la Kimataifa haikusikilizwa wala kufanyiwa kazi bali mapigano
ndio yakazidi kupamba moto zaidi !. Baada ya Ghadafi kuonyesha kutoheshimu
maamuzi ya baraza la usalama ambalo lilimtaka asitishe vita dhidi ya raia wake
na akakaidi, ndipo ule Muungano wa Atlantiki ya Kaskazini (NATO) ulipotumia fursa hiyo kuivamia Libya kwa kisingizio cha kuwalinda raia wa Libya wanaouliwa na majeshi ya
Ghadafi, lakini kabla ya kuivamia Libya kwanza walianza kwa kumzuia na kumuonya
Ghadafi kwa kumuonyesha 'taa nyekundu' iliyoashiria
marufuku ndege zake za kivita kuruka juu ya anga la Libya.
Muda mfupi baadae wanachama wa NATO
baada ya kuona Ghadafi haonyeki , ndipo walipo amua kukubaliana
kuiongezea Libya vikwazo vya ununuzi wa silaha, hiyo haikutosha
wakaamua kufanya Operesheni ya pamoja ya ulinzi
wa anga la Libya hasa baada ya kuona Ghadafi anaendelea kulitumia
anga kutoa mashambulizi kwa wapinzani wake.
Wanachama wa NATO waliamua kutoa
meli za kivita zilizobeba silaha za kivita, nyambizi na
zananyingine za kivita pamoja na ndege za kivita ili kujiweka tayari
kuelekeza mashambulizi yao ya pamoja nchi Libya na hasa lengo lao kubwa
likiwa ni kulinda anga la Libya lisitumike
dhidi ya wapinzani wanaodai demokrasia, na
ili kuzuia mamluki na maaskari wa kukodiwa
kutoka nchi jirani zinazoizunguka Libya, ambapo walikuwa wakiingia
Libya kupigana kwa ajili ya maslahi ya Muammal Ghadafi lakini pia nawao wakipokea
ujira mnono kwa kazi hiyo.
sehemu aliyouawa kanali Gadafi |
Nchi za kwanza kuingia Libya kwa
ajili ya operesheni hiyo ni
Marekani,Uingereza,Kanada na nyingine
zikiongozwa na Ufaransa.Ziliweza
kujitanua katika anga la Libya bila wasi wasi na kushusha majumba kadhaa ya
serikali ya Libya na ya wananchi wa kawaida,yaliweza kuua raia wengi
zaidi , yaliweza kulenga sehemu muhimu za kijeshi na kubomoa bomoa sehemu nyeti
za kiuchumi, na kuleta hasara kubwa.
Hatua hiyo ilijaribu kupunguza nguvu
za majeshi yanayomtii Ghadafi na hapo wapinzani wanamapinduzi wakapata fursa ya
kusonga mbele na kuteka miji kadhaa iliyokuwa chini ya uthibiti wa serikali ya
Ghadafi,maana upinzani waliokuwa wakikabiliana nao kutoka kwa majeshi ya
Ghadafi hasa baada ya kushindwa kulitumia anga kushambulia, ulikuwa hafifu
sana.
(Wapinzani wa Ghadafi na wanamapinduzi
wa Libya wakishangilia kwa kuukomboa Mkoa wa Benghazi -Machi 21,2011.)
Hali hiyo ilimghadhabisha sana ghadafi akanuna na kuapa kulipiza
kisasi na hizi ni picha zake zikidhihirisha ghaddhabu zake !.
( Gaddafi wants 'revenge).
Tarehe 24 mwezi wa Machi , NATO
'ilikubali' kuchukua uthibiti wa eneo rasmi ili kuongoza operesheni
iliyokwenda kwa ajina la "No-fly zone" 'Hakuna kuruka juu ya
anga'.Hivyo majukumu ya ule muungano wa mwanzo uliokuwa chini ya uongozi wa
ufaransa,NATO ikakubali kuyabeba kwa maana nyingine NATO akawa ndiye kiongozi
wa operesheni hiyo ili kutekeleza 'azimio la baraza la usalama' nchini Libya na
sio tena Ufaransa kama nchi inayojitegemea.
NATO -baada ya kukubali kubeba majukumu-ilianza rasmi kutekeleza
operesheni hiyo ya jeshi la anga tarehe 27 machi 2011,
huku nchi kadhaa za kiislaam
zikihaidi kujiunga na NATO katika operesheni hiyo dhidi ya Libya ambapo
zilizoonyesha kuwa mstari wa mbele kutekeleza ahadi hiyo ni pamoja na Qatar na
Falme za Kiarabu au "United Arab Emirates". Qatari inashiriki kwa
kuchangia au kwa kutoa ndege sita za kivita zinazokwenda kwa jina la 'Mirage
2000-5EDA fighter jets'na kutoa ndege moja kijeshi ya usafirishaji inayoitwa
C-17,wao ndege hii huiita:'C-17 military transport aircraft'.Na hii ni katika
kuchangia kutekeleza ile 'marufuku' ya urukaji wa ndege juu ya anga la Libya
kwa mujibu wa azimio la Balaza la Usalama la Kimataifa.Falme za Kiarabu au
United Arab Emerates wao wamekwisha tuma ndege za kivita sita zinazoitwa:F-16
Falcon na nyingine sita zinazoitwa: "Mirage 2000 fighter jets " ili
kujiunga na Operesheni hiyo ya kijeshi.Ndege hizo za Emirates zilitumwa tarehe
24 machi,2011.
Marekani imepeleka kikosi cha majini,meli za kivita 11,manowari
kadhaa,makombora kadhaa,na masiha mengine mazito mazito kama vile The
gui-missile Destroyers,USS Barry na USS Stout pamoja na USS Sranton,
hawakusahau pia kupeleka meli inayoitwa:'The amphibious command ship' na 'USS
Mount Whitney'.Wameongeza zaidi kwa kupeleka silaha zinazoitwa:B-2 Stealth
Bombers,AV-8B Harrier II kwa ajili ya mashambulizi ya ardhini ikiwa
yatahitajika,EA-18 ,F-15,na F-16 pamoja na wanajeshi kadhaa waliokwisha tumwa
kujiunga katika Operesheni hiyo dhidi ya Libya.
(B-2 ya Marekani ikijiandaa
ku-Land ili-kupumzika baada ya kutoa dozi ya kubomoa huko-Libya).
( USAF C-17A).
Italy nayo inashiriki kwa kutoa ndege za kivita na silaha
nyingine,pia imetoa Bases (au Maeneo) nyingi zaidi kuliko nchi nyingine
zilizoshiri katika operesheni hii,na hii ni kwa ajili ya "kuhifadhia
zana za kivita na ndege za kivita".maeneo hayo yanayoitwa: "Italian
airbase" ni haya yafuatayo:
Kuwait na Jordan nazo zitatoa "Mchango wa vifaa" kwa
mujibu wa kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon.
(Kuwaiti Mirage
2000C -fighter -aircraft).
German hiyo haitaki na imekataa kushiriki katika Operesheni hiyo
dhidi ya Libya na imetaka majeshi yote ya NATO kuondoka katika bahari ya
Mediteranian na kuachana na operesheni
hiyo dhidi ya Libya.China na Rushia pia zimepinga operesheni hiyo na kutaka
vita isimamishe mara moja kabla damu ya walibya kumwagiza zaidi na vita
kuwa mbaya zaidi wakitahadharisha Libya isijekugeuka na kuwa kama Iraq na Afghanistan.
Uturuki nayo itashiriki katika operesheni hii ya NATO kwa kutoa meri
tano na Manowari moja iliki kutekeleza vikwazo vya silaha
vilivyowekwa dhidi ya Libya.Lakini bado inafanya
uchunguzi zaidi wa vita hii na inatoa wito kwa Ghadafi ajiudhuru ili
kuepusha mauaji. Operesheni hii bado inaendelea na mapigano nchini libya kati
ya wanamapinduzi na wanakupinduliwa bado pia yanaendelea.
Operesheni hii ya NATO imezidisha
kasi ya mauaji kuliko hata kabla ya operesheni!,hii ni kwa mujibu wa uchambuzi
wa wataalamu wa masuala ya kivita na wasomi mbali mbali wa dunia pampja na nchi
kadhaa zinazosisitiza migoro ya nchi kama hiyo itatuliwe kwa njia ya mazungumzo
nasio mtutu.Lakini kwa kuwa hatumiriki elimu ya ghaibu,ngoja tusubirie hatima
ya nchi hii itakuwaje ili tukamilishe historia ya operesheni hii ya NATO kama
historia ya operesheni zake nyingine ilivyokamilika.
Tunawaombea walibya mafanikio na
wapate utulivu katika nchi yao.Mungu ibariki Africa,Mungu ibariki Libya.
Karibu kukubatacamp.
No comments:
Post a Comment