Havana, Kuba - 08/08/2010. Rais wa zamani wa Kuba Fidel Castro,
amehutubia taifa kwa mara ya kwanza tangu alipo achia madaraka ya uongozi.
Fidel Castro 83 amabye mpaka sasa ni
kiongozi wa chama Commnist alionya ya kuwa dunia inaelekea kwenye mashindano ya
kivita ambapo matumizi ya nyuklia huenda ya katumika.
Na alisema "Uongozi wa serikali
ya Amerika unampango wa kuzishambulia Iran na Korea ya Kaskazini, vilevile
ikiwa rais wa Amerika Baraka Obama atatoa ruhusa ya kuanza vita,basi watu wengi
watateketea wakiwemo Waamerika wanao fanya kazi katika maeneoya Mashariki ya
Kati,na huo utakuwa ndiyo mwisho wa kuwa na amri moja ya kidunia na kuleta
mgongano mkubwa kwenye maeneo ya Mashariki ya Kati na kwingine kote
duniani."
Vilelevile Fidel Castro alisema
" swala la mkubwa mmoja kutoa amri litafikia mwisho na baadhi ya miundo
mbinu ya kibiashara na fedha zita hathirika na kuangamia."
Pichani anaonekana aliye kuwa rais
wa Kuba Fidel Castro akihutubia mkutano hivi karibuni jijini Havana.
No comments:
Post a Comment