Ellen Johnson-Sirleaf (alizaliwa 29 Oktoba 1938
nchini Liberia) amekuwa rais wa kwanza mwanamke barani Afrika baada ya kushinda katika uchaguzi wa mwaka 2005. Johnson-Sirleaf ameshika
nyadhifa mbalimbali serikalini na katika mashirika ya kimataifa. Baada ya
kumaliza masomo katika chuo kikuu cha Harvard, alifanya kazi katika
serikali ya RaisWilliam Tolbert mwaka wa 1970 akiwa ni
Waziri wa Fedha.
Johnson amekuwa Rais wa
kwanza mwanamke barani Afrika. Hata hivyo yeye sio
mwanamke wa kwanza kuongoza nchi barani Afrika. Malikia
Zauditu wa Ethiopia aliongoza nchi yake kwa
miaka 13 toka mwaka 1917 hadi 1930. Ruth
Perry ni mwanamke wa kwanza Afrika kuwa mkuu wa
nchi pale alipokuwa mwenyekiti wa urais wa pamoja wa jamhuri ya Liberia toka
mwaka 1996 hadi 1997.
Johnson-Sirleaf alihukumiwa
kifungo cha miaka kumi jela mwaka 1985 baada ya kushutumu utawala wa kijeshi
nchini humo katika kampeni zake za kugombea ubunge. Alitumia kifungo hicho kwa
muda mfupi kabla ya kuachiliwa na baadaye kukimbilia uhamishoni hadi aliporudi
mwaka 1997 akiwa anafanyia kazi Benki
ya Dunia na Citibank.
Johnson-Sirleaf alimuunga
mkono Charles Taylor wakati wa mapinduzi yake
dhidi ya Jenerali Samuel Doe lakini baadaye alikuja kuwa
mpinzani wake mkubwa na hata kugombea urais dhidi yake mwaka 1997. Taylor
alimwandana na hata kumpeleka mahakamani kwa madai ya kuhusika na hujuma za
kihaini.
Uchaguzi wa urais mwaka
2005 ulirudiwa baada wagombea urais kutopata kura za kutosha. Katika raundi ya
kwanza Johnson-Sirleaf alikuwa wa pili, wa kwanza alikuwa ni mpinzani wake
mkubwa George
Weah.
Katika raundi ya pili ya uchaguzi, Johnson-Sirleaf alitangazwa kuwa mshindi.
Hata hivyo, George Weah amepeleka mashtaka mahakama kuu akidai kuwa uchaguzi
haukuwa wa haki.
Wasifu
Ellen Johnson Sirleaf
alizaliwa mjini Monrovia, mji mkuu wa Liberia, na elimu ya wazazi. Kabila lake
ni nusu Gola kutoka upande wa baba yake, na robo Kru na robo Kijerumani kutoka
upande wa mama yake. Babake Sirleaf Jahmale Carney Johnson, alikuwa mzaliwa wa
Liberia wa kwanza kuweza kukaa katika mbunge la taifa. Sirleaf alisoma maswala
ya uchumi na akaunti katika Chuo Afrika Magharibi mjini Monrovia. Aliolewa na
James Sirleaf akiwa na miaka 17 tu na kuhamia Marekani katika mwaka wa 1961
ambapo aliendelea na masomo yake katika chuo kikuu cha Colorado na kuhitimu na
shahada ya digri. Alisomea maswala ya uchumi na sera za umma katika chuo Chuo
Cha Maswala Ya Serikali ya John F. Kennedy, mjini Harvard katika miaka ya 1969
na 1971 na kupata shahada ya maswala ya serikali. Kisha alirudi Liberia na
kufanya kazi chini ya rais William Tolbert. Alikuwa naibu waziri wa fedha kati
ya mwaka wa 1972 na 1973. Alikuwa waziri wa fedha toka mwaka wa 1979 hadi
Aprili 1980. Aliweza kuwa naibu mwenyekiti wa benki ya CitiBank mjini Nairobi,
Kenya kutoka mwaka wa 1983-1985. Aliwahi kufungwa mafungo ya nyumbani na Samule
Doe aliyepindua serikali kwa kutangaza nia ya kugombea urais. Baadaye alienda
uhamishoni. Kati ya miaka ya 1986-1992 alikuwa makamu wa rais na mwanachama wa
bodi ya benki ya Equator, Washington, DC. Kati ya miaka ya 1988-1999 alikuwa
mbunge wa bodi ya wakurugenzi wa Taasisi ya Synergos. ALigombea urais kwa
tiketi ya chama ya maungano(Unity Party) katika mwaka wa 1997 na kuwa
Urais
Ndiye rais wa sasa wa Liberia.
Alimshinda alikuwa mwanasoka mashuhuri George Weah na zaidi ya asilimia
ishirini katika uchaguzi wa mwaka wa 2005. Uzinduzi ulifanyika tarehe 16
Januari 2006 na ulihudhuriwa na wageni mashuhuri wakiwemo aliyekuwa waziri ya
maswala ya kigeni wa Marekani, Condeleeza Rice, Laura Bush na Mitchelle Jean.
Katika mwaka wa 2005 alianzisha tume ya ukweli na maridhiano ambayo ilitoa
ripoti yake katika mwaka wa 2009.
No comments:
Post a Comment