Ndege ya kivita ya Iran
imeitimua ndege ya kijasusi isiyo na rubani (drone) ya Marekani ilikyokuwa
ikiruka katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
Hayo yamethibitishwa na George
Little, afisa wa habari katika Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon.
Akizungumza siku ya Alkhamisi, Little amesema tukio hilo lilijiri tarehe 12
mwezi huu wa Machi wakati ndege isiyo na rubani ya Marekani ilipokuwa ikifanya
'ujasusi wa kawaida' katika eneo la Ghuba ya Uajemi. Amesema ndege ya kivita ya
Iran aina ya F-4 iliifuata drone hiyo ambayo ilikuwa ikiruka karibu na ndege
zingine mbili za kivita za Marekani. Hivi karibuni pia Kamanda wa Kituo cha
Ulinzi cha Khatam al-Anbiya nchini Iran, Brigedia Jenerali Farzad Esmaili
alisema vikosi vya ulinzi nchini vilifanikiwa kuitambua na kuitimua ndege ya
kijasusi ya Marekani aina ya U2 ambayo ilikuwa ikijaribu kuingia katika anga ya
Iran kwenye eneo la Bahari ya Oman. Alisema mnamo Februari 10 mwaka huu, mfumo
wa ulinzi wa anga wa Iran ulifanikiwa kuigundua na kuitimua ndege hiyo ya
kijasusi ambayo ina uwezo wa kukwepa rada. Kwa mara kadhaa sasa hivi karibuni
vikosi vya ulinzi vya Iran vimefanikiwa kunasa ndege za kisasa kabisa za
kijasusi za Marekani kama vile ScanEagle na RQ-170 Sentinel.
CHANZO : Sauti ya Iran.
No comments:
Post a Comment