Mnamo august 1983, vijana wawili, makapteni wa jeshi na wanamapinduzi, Thomas sankara na blasius compaore, walipindua serikali ya rais wa wakati huo katika nchi iliyojulikana kama upper volta, rais huyu aliitwa Baptiste Ouedraogo.
Vijana hawa wakiwa katika fikra za kimax, wakiwa na ndoto nyingi za kuijenga upper volta, walibadili kabisa historia ya taifa hilo, walibadili jina la nchi na kuitwa Burkina faso, manake nchi ya watu, country of honorable citizen.
Uchapa kazi wa vijana hawa , Thomas sankara akiwa ndiye rais unaweza kufananishwa na ule wa Fider Castrol na Che Guavera, kabla haujachuja.
Haiyumkini sankara alikuwa anatumia baiskeli kutembelea vijijini kuhimiza maendeleo, wakati pacha wake compaore wakiwa kama pete na kidole.
Urafiki wa makapteni hawa ulikuwa mkubwa kiasi ambacho, wakati wanausalama walipomwambia sankara kuwa compaore ana mpango wa kumpindua na kumuua, yeye aliwajibu kuwa compaore asingeweza kufanya hivyo, labda mtu mwingine.
Akaongeza kuwa hata kama compaore angetaka kufanya hayo, hakuna wa kumzuia. Ni wazi kuwa sankara alikuwa karibu mno na compaore,kwa kiasi kuwa compaore alikuwa sehemu ya maisha ya kila siku ya sankara.
kama ilivyotabiriwa, compaore aliongoza mapinduzi yaliyosababisha kifo cha sankara mwaka 1987, na yeye mwenyewe huku akishuhudia rafiki yake kipenzi sankara akiuuwa, Akawa ndo rais.
Isidire Thomas Sankara alizaliwa tarehe 12.12.1949 Mjini YOKO (Volta ya juu) na kuuawa tarehe 15.10.1987 na wanajeshi wenzake wakiongozwa na rafiki yake Rais Blaise Compaore katika mapigano ya usaliti yaliyotokea Mjini Ouagadougou akiwa katika kikao cha utendaji wa kazi.
Mwaka 1981 alikuwa waziri wa mambo ya ndani katika serikali ya kijeshi ya Rais Jean Baptiste Major. Dr. na baadaye aliteuliwa kuwa waziri mkuu kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Januari 1983 mpaka mwezi Mei alipokamatwa na kutiwa mbaroni na serikali ya Rais Major Jean Baptiste Dr kutokana na msimamo wake juu ya ukombozi kwa watu wote wa Volta na kupendelea Marxist Revolution theories.
Thomas Sankara alikuwa Rais kuanzia mwezi Agosti 4. 1983 hadi mwezi Octoba 15 1987 baada ya mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Major Dr Jean Baptiste yakiongozwa na Blaise Compaore na kuwa Rais wa TANO wa VOLTA YA JUU au BURKINA FASO
Thomas Sankara aliyejulikana kama Che – Guevara wa Afrika alianzisha Program mbalimbali za kijamii na kiuchumi kuleta mabadiliko katika nchi za afrika. Alibadilisha Upper Volta na kuwa Burkina Faso (land of Upright Men’’)
Alianzisha kampeni ya kuboresha Elimu na kutanua
Huduma za Afya kwa watu wa Burkina Faso hasa kwa
watoto walio athirika na magonjwa ya Uti wa mgongo
, Homa ya majano na kampeni ya upandaji wa miti
kitaifa takribani Milioni kumi.
1. Aliongeza
idadi ya wanawake katika serikali yake, kupinga tohara kwa wanawake, kuwataka
wanawake waliopata mimba wakiwa mashuleni kuendelea na masomo.
Thomas sankara Taa iliyozimika gafla akiwa na umri mdogo wa miaka 38 ndoto zake za kuifanya Burkina Faso kuwa taifa lenye uchumi mpana, serikali inayotoa haki kwa watu wote, zilifutika mapema sana tarehe 15 mwezi wa Kumi 1987 baada ya kuuawa na Rafiki yake Blaise Compaure na washirika wake. Wiki moja kabla ya kuuawa alisema maneno haya... “While Revolutionaries as individuals can be murdered, you cannot kill Ideas”
Afrika itakukumbuka Daima Thomas Sankara Pumzika kwa amani ya Bwana. FIKRA NA MAWAZO YAKO VITAISHI DAIMA
“Father land or Death, we will win”
“He who feeds you, Controls you”
The revolution and women’s liberation go together. We do not talk of women’s emancipation as an act of charity or because of a surge of human compassion. It is a basic necessity for the triumph of the revolution. Women hold up the other half of the sky. Thomas Sankara Thomas knew how to show his people that they could become dignified and proud through will power, courage, honesty and work. What remains above all of my husband is his integrity. Mariam Sankara, Thomas' widow
Che Guevara taught us we could dare to have confidence in ourselves, confidence in our abilities. He instilled in us the conviction that struggle is our only recourse. He was a citizen of the free world that together we are in the process of building. That is why we say that Che Guevara is also African and Burkinabè. Thomas Sankara
Chanzo : kutoka katika mitandao
Thomas Sankara will be remembered by those who knew his great plan to Burkina Faso. He wanted to let people of Burkina Faso to enjoy the cake of their country
ReplyDelete