Friday, January 31, 2014
INDIRA GANDHI
Leo hii niko
hai pengine kesho inawezekana nisiwe hapa. Nitaendelea kuwatumikia wananchi wa
India mpaka pumzi yangu ya mwisho. Na kama nikifa,kila tone la damu yangu
litajenga muungano usiofutika.
Hayo ni
baadhi ya maneno ya waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa India, bibi Indira Ghandi
katika hotuba yake ya mwisho,siku moja
kabla ya kuuawa, oktoba 30 mwaka 1984. Hoja nyingi zilijengwa ndani na
nje ya ya india baada ya hotuba yake ya mwisho,huku wengi wakiyatafsiri maneno
yake kama utabiri wa kifo chake siku moja baadae.
Uzito wa
maneno hayo ulitimia siku moja baadaye,kwani alipoteza maisha kwa shambulio la
risasi kutoka kwa walinzi wake. Oktoba 31 mwaka 1984,walinzi wawili wa
Gandhi,Satwant Singh na Beant Singh,walimfyatulia risasi mwanamama huyo wakati
akitembea kwenye bustani yake iliyopo barabara ya 1 Safdarjung Road,New Delhi.
Gandhi
alipigwa risasi wakati akielekea kwenye mahojiano na mcheza filamu wa England,
Peter Ustinov,ambaye lengo la mahojiano hayo ilikuwa ni kuandaa kipindi maalumu
documentary. Singh alifyatua risasi tatu kwa Ghandhi huku mwenzake Satwant
akifyatua risasi zisizofahamika idadi.
Baada ya kuhakikisha wamekamilisha
mauaji,walinzi hao walijisalimisha. Baada ya hapo walipelekwa kwenye chumba
maalumu kwa ajili ya kuhojiwa, ambapo Bent Singh alipigwa risasi,huku mwenzake
akihukumiwa adhabu ya kunyongwa kwenye jela ya Tihar.
Uchunguzi wa mwili wa
Gandhi uliofanywa kwenye kituo cha sayansi na tiba,india alikopelekwa baada ya
kuondolewa sehemu ya tukio,ulithibitisha kifo chake kutokea baada ya kupigwa
risasi 30 sehemu mbalimbali mwilini.
Gandhi alitangazwa amefariki dunia saa 10
baadaye,ingawa taarifa za awali zilidai kuwa alifariki siyo zaidi ya dakika
moja baada ya kushambuliwa kwa risasi. Kuna sababu nyingi zimeelezwa zikihusishwa
na kifo cha Gandhi,
lakini kubwa inayotajwa ni chukio la kundi la uasi la
Kalasinga la mjini Punjab,India lililochukizwa na uamuzi wa Gandhi kuamuru
jeshi liwashambulie.
Inadaiwa kuwa Gandhi alitoa amri kwa jeshi kuvamia hekalu
la kalasinga walikokuwa wamejificha waasi wenye silaha,na baada ya shambulizi
kufanyika haukupita muda mrefu Gandhi akauawa na walinzi wake.
Indira Gandhi
alizaliwa November 19 mwaka 1917. Ni waziri Mkuu wa kwanza mwanamke nchini
India. Indira alizaliwa kama binti wa Jawaharial Nehru,aliyekuwa waziri mkuu wa
kwanza wa India kati ya mwaka 1947 hadi 1964.
Jina la Gandhi alipokea kwa njia
ya ndoa na Feruz Gandhi ambaye hakuwa na uhusiano na Mahatma Gandhi.
Alishirikiana na baba yake kama karani katika shughuli zake za kisiasa na ilipofika
mwaka 1955, alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha congress.
Baada ya kifo cha
baba yake, mzee Nehru aliingia katika serikali kama waziri, na baadaye
akachaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1966 akatawala hadi 1977 mwaka 1980
alirejea madarakani tena na kushika uongozi wa juu,na ni katika kipindi hicho
ulipotokea uasi uliosababisha kukosekana kwa amani kabla ya kuamuru nguvu ya
jeshi kutumika,. Siku chache baada ya kuuawa,mtoto wake wa kiume Rajiv
Gandhi,akatawazwa kuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 1984 mpaka 1989 alipouawa kwa
bomu la kutegwa.
Wednesday, January 29, 2014
IRAN YAIFUKUZA NDEGE YA KIJASUSI YA MAREKANI
Ndege ya kivita ya Iran
imeitimua ndege ya kijasusi isiyo na rubani (drone) ya Marekani ilikyokuwa
ikiruka katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
Hayo yamethibitishwa na George
Little, afisa wa habari katika Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon.
Akizungumza siku ya Alkhamisi, Little amesema tukio hilo lilijiri tarehe 12
mwezi huu wa Machi wakati ndege isiyo na rubani ya Marekani ilipokuwa ikifanya
'ujasusi wa kawaida' katika eneo la Ghuba ya Uajemi. Amesema ndege ya kivita ya
Iran aina ya F-4 iliifuata drone hiyo ambayo ilikuwa ikiruka karibu na ndege
zingine mbili za kivita za Marekani. Hivi karibuni pia Kamanda wa Kituo cha
Ulinzi cha Khatam al-Anbiya nchini Iran, Brigedia Jenerali Farzad Esmaili
alisema vikosi vya ulinzi nchini vilifanikiwa kuitambua na kuitimua ndege ya
kijasusi ya Marekani aina ya U2 ambayo ilikuwa ikijaribu kuingia katika anga ya
Iran kwenye eneo la Bahari ya Oman. Alisema mnamo Februari 10 mwaka huu, mfumo
wa ulinzi wa anga wa Iran ulifanikiwa kuigundua na kuitimua ndege hiyo ya
kijasusi ambayo ina uwezo wa kukwepa rada. Kwa mara kadhaa sasa hivi karibuni
vikosi vya ulinzi vya Iran vimefanikiwa kunasa ndege za kisasa kabisa za
kijasusi za Marekani kama vile ScanEagle na RQ-170 Sentinel.
CHANZO : Sauti ya Iran.
Subscribe to:
Posts (Atom)