Matumizi ya silaha katika jamii ya
Wazayuni, yamewatia tumbo joto viongozi wa utawala wa Israel kutokana na
kuongezeka kwa vitendo vya jinai na kukosekana kwa utulivu huko katika ardhi za
Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Kuhusiana na suala hilo, hapo jana gazeti la
Kizayuni la Haaretz liliandika kuwa, karibu silaha zipatazo laki mbili na
tisini elfu zipo mikononi mwa wakazi wa utawala huo bandia, ambapo kati ya hizo
silaha laki moja na 57 elfu zinamilikiwa wa walowezi wa Kiyahudi huku nyingine
laki moja na 30 elfu zikiwa mikononi mwa vyombo vya usalama vya utawala huo.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na gazeti hilo, tangu mwaka 2002 hadi sasa
wanawake wapatao 16 wa Kizayuni wamekwishauliwa na waume zao kwa kutumia silaha
hizo moto. Aidha gazeti hilo limeeleza kuwa, mbali na askari wa Kizayuni
kutumia silaha katika maeneo yao ya kazi, huzihifadhi silaha hizo majumbani
mwao, suala ambalo linazidi kuhatarisha jamii ya Wazayuni. Gazeti la Kizayuni
la Haaretz limeandika kuwa, kwa ujumla hakuna usimamizi wala udhibiti wowote
unaofanywa kuhusiana na silaha zinazowekwa katika makazi ya askari wa Kizayuni
suala ambalo limepelekea askari hao kuzitumia katika vitendo visivyo vya
kijeshi kama vile wizi na kadhalika. Matumizi ya silaha katika jamii ya
Kizayuni na kuruhusiwa raia wengi wa utawala huo kubeba silaha hizo, kunajiri
katika hali ambayo vitendo vya ukatili na uhalifu mbalimbali wa jinai umegeuka
na kuwa tatizo sugu kwa jamii ya utawala wa Israel. Alaa kulli hali, kushadidi
mwenendo wa utumiaji silaha katika jamii ya Kizayuni na ambao unahesabiwa kuwa
mgogoro wa ndani wa utawala wa huo, kunaakisi jinai mbalimbali ambazo
zinafanywa na utawala wa Tel Aviv dhidi ya nchi mbalimbali za ulimwengu. Kwa
upande mwingine, kuruhusiwa matumizi ya silaha huko Israel, kuna maana kwamba,
utawala huo hauna uwezo wa kuwadhaminia usalama raia wake na kwamba, raia hao
ndio wanaopaswa kujilinda wenyewe kwa kutumia silaha hizo. Hata hivyo badala ya
silaha hizo kuleta amani na usalama, zimezusha vitendo vya ukatili, machafuko
na uasi katika jamii ya Wazayuni. Hakuna shaka kwamba, kushadidi hali ya
machafuko katika jamii ya Israel, ni moja ya sababu zilizopelekea kuongezeka
kwa kasi hali ya uhamaji wa Wazayuni kutoka ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa
mabavu, kwani Mayahaudi hao hawako tayari kuishi katika jamii iliyojaa jinai na
machafuko. Inasemekana kuwa, viongozi wa utawala wa Kizayuni sambamba na kutoa
ahadi za uongo kuhusiana na kuwepo pepo iliyoahidiwa kwa ajili ya Mayahudi huko
Palestina, wanatumia kila njia ili kuwashawishi Wazayauni kuhamia katika ardhi
hizo wanazozikalia kwa mabavu. Hata hivyo Mayahudi hao hukumbana na hali iliyo
tofauti kabisa na ahadi hizo mara tu wanapowasili huko.
No comments:
Post a Comment