KUKUBATACAMP
Sunday, August 3, 2014
HABARI MBALIMBALI
Laurent Gbagbo akutana na viongozi wa ECOWAS.
Abidjan, I Marais watatu wa jumuia ya
kiuchumi ya nchi za Afrika ya Magharibi wamekutana na rais wa Ivoty Coast ili
kujadili hali ya kisiasa nchini humo na kumtaka aachie madaraka. Marais hao ni
Boni Yayi wa Benin, Ernest Bai wa Sierra Leone, na Pedro Pires wa Kape Verde
walikutana na rais wa sasa Laurant Gbagbo kuzungumzia hali halisi ya myumbo wa
kisiasa uliopo katika nchi hiyo. Marais hao kabla ya kuonana na Gbagbo,
waliongea na Alassane Ouattara ambaye jumuia ya kimataifa inamtambua kama ndiye
mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika hivi karibuni. Hata hivyo hakuna
habari zilizo tolewa kwa undani ili kwa pamoja walisema mkutano ulikuwa wa
mafanikio. Picha hapo juu wanaonekana marais wa Laurent Gbagbo kushoto, Ernest
Bai Koroma wa Sierra Leone na Boni Yayi wa Benin wakiongea na waandishi
wahabari mara baada ya kukutana kwao.
Urussi
yazitaka nchi nyingine kuangalia mambo yao.
Moscow, Urussi Serikali ya Urussi imezitaka serikali za nchi nyingine kutoingilia
mambo yake na nchi hizo zitizame maswala ya nchi zao.
Uamuzi wa serikali ya Urussi kutoa
tamko hilo umekuja mara baada ya baadhi ya nchi zikiongozwa na Amerika kulaumu
kitendo cha mahakama nchini Urussi kumkuta na hatia Mikhail Khodorkovsky kwa
kosa la kutumia mali na pesa za nchi kinyume cha sheria .
Waziri wa mambo ya nje wa Amerika
Hillary Clinton, alisema " kitendo cha kuhukumiwa kwa Mikhail kinaleta
mashaka kutokana na jinsi kesi hiyo ilivyo endesshwa."
Picha hapo juu anaonekana Mikhail
Khodorkovsky akisikiliza hukumu ilipo kuwa inatolewa mbele yake.
Makampuni
ya Amerika yafanya biashara za kijamii na Iran.
New York, Wizara ya biashara ya Amerika imetoa
vibali kwa makampuni ili kufanya biashara nchini Iran kwa kipindi cha miaka
kumi iliyo pita.
Kwa mujibu wa habari zilizo patikana
vibali vipatavyo 10,000 vilitolewa kwa makampuni maalumu ili kufanya biashara
za kusaidia jamii. Moja ya makampuni hayo ni Kraft Food, Pepsi na baadhi ya
biashara za kibenki ambazo zilikuwa zinasaidia jamii katika maendeleo. Stuart
Levey, msimamizi wa maswala ya vikwazo alisema " hii inafanyika
kuhakikisha ya kuwa vikwazo visiathili watu hata wakafikia kukusa vyakula
ambapo haitakuwa jambo la kiutu." Serikali ya Amerika iwekea Iran vikwazo
ili nchi hiyo iweke wazi ukweli wake kuhusu mpango mzima wa mradi wake wa
kinyuklia jambo ambalo Iran inalipinga na kukataa katakata kufanya hivyo. Picha
hapo juu ni picha ya moja ya kampuni ambayo imewekeza kibiashara nchini Iran.
Korea ya Kusini na Kaskazini wasiwasi wazidi kukuwa. Seoul, Korea ya Kusini Serikali ya Korea ya Kusini inaamini ya kuwa serikali ya Korea ya Kaskazini huenda ikafanya majaribio ya bomu la nyuklia mapema mwakani. Kutikana na ripoti kutoka wizara ya mabo ya nje ya Korea ya Kusini zinasema "majaribio hayo yatafanywa na Korea ya Kaskazini ikiwa ni njia moja wapo ya kukuza na kuangalia uwezo wa wake wa nguvu za Kinyuklia. Na majaribio hayo yatasababisha hali kuwa ya wasiwasi zaidi kati nchi hizo mbili." Korea ya Kaskazini ilifanya majaribio tofauti ya kinyuklia mwaka 2006 na 2009 kwa mujibu wa habari zinazoeleweka kimataifa, lakini Korea ya Kaskazini yanyewe haijawai kutamka kuhusu swala hilo. Picha hapo juu anaonekana mmoja wa mwanajeshi wa Korea ya Kaskazini akiwa katika moja ya vituo vilivyopo mpakani na Korea ya Kusini tayari kwa kazi ya ulinzi huku akiwa ameelekeza bundiki tayari.
ECOWAS uenda ikatumia nguvu nchini Ivory Coast. Abidjan, Ivory Coast - Viongozi wa shirikisho la uchumi wa Afrika ya Magharibi (ECOWAS) wamemtaka rais wa sasa wa nchi hiyo kuachia madaraka mara moja. Viongozi wa shirikisho la ECOWAS walisema "ikiwa rais Gbagbo hatafanya hivyo basi itabidi nguvu zaidi itumike." Agizo hilo lilitolewa na viongozi wa ECOWAS lenye nchi wanachama 15 wakati walipo kutana jijini Abuja kujadili hali halisi ya Ivory Coast. Vurugu za kisiasa nchi Ivory Coast zilizidi mara baada ya matokeo ya uchaguzi wa rais kutangazwa na rais Laurant Gbagbo kudai ya kuwa ameshinda na huku mpinzani wake Alassane Ouattara akidai yeye ndiye aliye shida uchaguzi wa rais. Picha hapo juu anaonekana rais wa sasa wa Ivory Coast Laurent Gbagbo akiongea wakati wa kampeni zake za uchaguzi wa rias.
Korea ya Kusini na Kaskazini wasiwasi wazidi kukuwa. Seoul, Korea ya Kusini Serikali ya Korea ya Kusini inaamini ya kuwa serikali ya Korea ya Kaskazini huenda ikafanya majaribio ya bomu la nyuklia mapema mwakani. Kutikana na ripoti kutoka wizara ya mabo ya nje ya Korea ya Kusini zinasema "majaribio hayo yatafanywa na Korea ya Kaskazini ikiwa ni njia moja wapo ya kukuza na kuangalia uwezo wa wake wa nguvu za Kinyuklia. Na majaribio hayo yatasababisha hali kuwa ya wasiwasi zaidi kati nchi hizo mbili." Korea ya Kaskazini ilifanya majaribio tofauti ya kinyuklia mwaka 2006 na 2009 kwa mujibu wa habari zinazoeleweka kimataifa, lakini Korea ya Kaskazini yanyewe haijawai kutamka kuhusu swala hilo. Picha hapo juu anaonekana mmoja wa mwanajeshi wa Korea ya Kaskazini akiwa katika moja ya vituo vilivyopo mpakani na Korea ya Kusini tayari kwa kazi ya ulinzi huku akiwa ameelekeza bundiki tayari.
ECOWAS uenda ikatumia nguvu nchini Ivory Coast. Abidjan, Ivory Coast - Viongozi wa shirikisho la uchumi wa Afrika ya Magharibi (ECOWAS) wamemtaka rais wa sasa wa nchi hiyo kuachia madaraka mara moja. Viongozi wa shirikisho la ECOWAS walisema "ikiwa rais Gbagbo hatafanya hivyo basi itabidi nguvu zaidi itumike." Agizo hilo lilitolewa na viongozi wa ECOWAS lenye nchi wanachama 15 wakati walipo kutana jijini Abuja kujadili hali halisi ya Ivory Coast. Vurugu za kisiasa nchi Ivory Coast zilizidi mara baada ya matokeo ya uchaguzi wa rais kutangazwa na rais Laurant Gbagbo kudai ya kuwa ameshinda na huku mpinzani wake Alassane Ouattara akidai yeye ndiye aliye shida uchaguzi wa rais. Picha hapo juu anaonekana rais wa sasa wa Ivory Coast Laurent Gbagbo akiongea wakati wa kampeni zake za uchaguzi wa rias.
India
na Urussi kushirikiana kwa ukaribu zaidi.
New Delhi,
India - 21/12/2010. Serikali ya India na Urussi zimekubaliana kwa pamoja
kushirikiana katika nyanja za kiusalama na kutiliana mikataba ya kibiashara
uchumi na sayansi. Rais wa Urussi Dmirty Medvedev na waziri mkuu wa India
Manmohan Singh walikubaliana mikataba hiyo wakati walipo kutana na kuzungumza
ili kudumisha uhusiano zaidi. Ziara hiyo wa rais wa Urussi imekuja baada ya
ziara za kufuatana za viongozi wa Uingereza, Amerika, China na Ufaransa kufanya
ziarani nchini India ili kudumisha ushirikiano wakaribu. Picha hapo juu
wanaonekana rais wa Urussi Dmirty Medvedev kushoto akipeana mkono na waziri
mkuu wa India Manmouhan Singh mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao. Irak yapata serikali mpya.
Bagdad, Irak - 21/12/2010. Bunge la Iraki limekubaliana kwa pamoja
kupitisha uteuzi wa waziri mkuu wa Irak na serikali yake na kutegua kitendawili
cha kisiasa kilicho dumu zaid ya miezi tisa. Nouri al Maliki, ataiongoza
serikali serikali ya Irak kwa kushirikisha makundi yote ya kisiasa ya Shia Sunn
na Kurdi. Akiongea mara baada ya kupitishwa kwa serikali yake Nouri al Maliki
alisema, serikali yake itajitahidi kwa kwa kila hali kuongoza wananchi wa Irak
na ingawaje kwa sasa kunawakati mgumu ambao utasababisha baadhi ya mambo kuto
fikiwa malengo kama ya livyo pangwa ili kuinua maisha ya wa Irak. Picha hapo
juu anaonekana Nouri al Maliki kushoto akiwa na Ayad Allawi ambao hapo mwazo
misimamo yao tofauti ilisababisha mvutano wa kisiasa kwa muda mrefu na kuleta
wasiwasi mkubwa.
Jeshi la umoja wa mataifa kuendelea kuwepo Ivory Coast.
Jeshi la umoja wa mataifa kuendelea kuwepo Ivory Coast.
Abidjan, Ivory Coast. Umoja wa Mataifa umekibaliana kwa
pamoja kuendelea kuwepo kwa jeshi la Umoja la kulinda amani nchini Ivory Coast
kwa kipindi zaidi cha miezi sita.
Jeshi hili lenye wapiganaji wapatao
10,000 litakuwa na majukumu mengine ya ziada, ikiwa ni kulinda wanchi na
kupambana na mashambulizi ya aiana yoyote.
Uamuzi huo umechukuliwa baada ya
rais wasasa Laurent Gbagbo, kulitaka jeshi hilo kutoka nchini humo mara muda wa
makubaliana yaliyo wekwa utakapo kwisha.
Pia umija wa Ulaya na washiriki wake
wamemwekea vikwazo rais Gbagbo na washirki wake wakaribu.
Msemaji wa Ikulu ya Amerika, Robert
Gibbs alisema "inabidi Gbagbo aondoke madarakani mara moja."
Hata hivyo rais Laurent Gbagbo, bado
anashikilia kiti cha urais huku akiungwa mkono na jeshi kwa kusaidiwa na wadau
wake.
Picha hapo juu vinaonekana vifaru
vya umoja wa mataifa vikiwa vimesimamishwa nje ya ofisi ya umoja wa mataifa
iliyopo jiji Abidjan.
Baraka
Obama atangaza hali halisi ya Afghanistan.
Washington,
Amerika Serikali na washiriki wake wanafanya kazi nzuri katika
kuijengaAfghanistan na kuwaanda wananchi wa Afghanistan kuijenga nchi yao. Rais
Baraka Obama, alisema "ingawaje hali ni ngumu lakini hii siyo kikwazo
kwani, na nashukuru wale wote waliojitolea na kuendelea kujitolea pamoja na
wapiganaji wetu ambao wanafanya kazi usiku na mchana ili kuijenga
Aghanistan." Akiongezea rais alisema, "maendeleo yanaonekana na
maendeleo haya ndiyo msingi mkubwa wa kuwafanya wananchi wa Afghanistan kuamini
yakuwa kazi iliyo fanywa na jumuiya ya kimataifa ilikuwa ni kwa ajili ya
wanachi wa Afghanistan." Baraka Obama, ameongea hayo ili kuwahakikishia
wanachi wa Afghanistan ya kuwa Amerika ipo pamoja nao. Picha hapo juu
anaonekana rais Baraka Obama, akiongea na waandishi wa habari ili kuzungumzia
hali halisi ya Afghanistan na mipango ya kuisadia nchi hiyo kimaendeleo.
Hatimaye mwanzilishi wa Wiki Leaks akubaliwa dhamana
Hatimaye mwanzilishi wa Wiki Leaks akubaliwa dhamana
London, Uingereza - 15/12/2010.
Mahakama kuu jijini London imemwachia huru mwanzilishi wa Wiki Leaks baada ya
mahakama ya mwanzo kukataa kumwachia huru kutokana na rufaa iliyo mtaka
aendelee kukaa mahabusu.
Julian Assange 39 aliachiwa na
kusema ya kuwa "anawashukuru wale wote walio changia kwa kiasi kikubwa
hadi kuachiwa kwake na akasema ataendelea na kazi yake kama kawaida.
Assange anatakiwa Sweden kwa kosa la
kufanya mapenzi ya kuchutukiza na moja ya wanamama wakati alipo kuwa nchini
Sweden. Picha hapo juu anaonekana Julian Assange aliyeshikilia karatasi
akitokea ndani ya mahakamani mara baada ya masharti ya dhamana kutimilizwa.
Serikali ya Amerika kuishitaki kampuni ya mafuta ya BP.
Washington, Amerika . Serikali ya Amerika imefungua kesi
dhidi ya kampuni ya mafuta BP kutokana na uharibifu iliotokea baada ya mafuta
machafu kuharibu mazingira katika pwani za Ghuba ya Mexico.
Mwanasheria mkuu wa Amerika, Erik
Holder alisema, "uchafuzi wa mazingira ulio tokea ulisababishwa na BP
kutofatilia sheria na kukamilisha maswala ya kiafya na usalama katika uchimbaji
wa mafuta na tunaangalia ni kwa njia za kufanya ili kuhakikisha BP inawajibika
kwa kuvunja sheria ya kuweka maji kuwa safi ( Clean Water Act )."
Uamuzi wa serikali ya Amerika
kufuangua kesi dhidi ya BP, baada ya moja ya visima vyake kuvuja na kusambaza
mafuta machafu katika Ghuba ya Mexico.
Picha hapo juu inaonyesha moja ya
machafuko yaliyo sababishwa na mafuta machafu katika moja ya eneo la pwani ya
Ghuba ya Mexico.
China na
India kushirikiana kwa karibu zaidi.
New Dheli,
India - 15/12/2010. Waziri mkuu wa China amefanya ziara nchini India ili
kuendeleza uhusiano wa nchi hizo mbili.
Wen Jiabao amekutana na waziri mkuu
wa Manmohan Singh na kujadili maswala mbalimbali ya ushirikiano kati ya nchi
hizo mbili hasa katika kukuza biashara ambapo huenda ikafikiwa kiasi cha $ 100
Billion.
Ziara hiyo ya waziri mkuu wa China
nchini India inatafsiliwa kuwa imekuja wakati muafaka kwani India ni nchi
ambayo uchumi wake unakuwa kwa kasi. Waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, akikagua
gwaride lililo andaliwa wakati alipo wasili nchini India.
Hakimu, Duncan Ouseley alikataa
maombi ya mwana sheria wa serikali ya Sweden ya kutaka Julian Assange aendelee
kukaa mahabusu kwa madai ya kuwa "anaweza kukumbia."
Kuachiwa kwa Julian Assange,
kumewezekana mara baada ya wadau wake kuchangisha kiasi cha US dollar zipatazo
laki tatu na robo, chini ya uongozi wa watu mashuhuri kama Jemina Khan,Bianca
Jagger, Ken LOach na John Pilger.
Picha hapo juu anaonekana Julian
Assange akiingia mahakamani kusikiliza ombi la dhamana yake ambapo hapo mwanzo
alikataliwa na mahakama ya mwanzo.
Irak
yaondolewa vikwazo na Umoja wa Mataifa.
New York, Amerika
- 15/12/2010.Kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa imeiondolea vikwaza nchi ya
Irak iliyo kuwa imeviweka kwa muda wa zaidi ya miaka 19. Akiongea katika
mjadala wa kutaka kuiondolea vikwazo Irak, makamu wa rais wa Amerika Joe Biden
alisema "Irak inahitaji kuwa katika kiwango cha kimataifa kwa kujitegemea
yenyewe na demokrasi ndiyo msingi mkubwa ambo utifanya nchi hiyo imeze
kuendelea na Wairak wameonyesha uwezo huo. Pia ni muhimu kwa Irak kuwa na
uhusiano mzuri na majirani zake kwani bado Wairak wanamthian mkubwa
mbeleni." Katika kikao hicho, kamati ya usalama iliondo vikwazo vyote
ilivyoviweka kwa Irak na kupitisha mswada ambao umeiruhusu Irak kuweza kujenga
mtambo wa nyuklia kwa matumizi ya kawaida. Vikwazo kwa Irak viliwekwa mwaka
1991 na umoja wa Mataifa mara baada ya Irak kuivamia Kuwait mwaka 1990 enzi ya
utawala wa rais Saddam Huissen ambaye alitolewa madarakani na serikali ya
Amerika mwaka 2003 baada ya kushukiwa kuwa na siraha za kuangamiza jamii. Ghana kuanza kuzalisha mafuta. Akrah, Ghana -Wananchi wa Ghana kwa mara ya kwanza wameungana na nchi nyingine
dunia katika kuzalisha mafuta kutoka kwenye Ghuba ya Guinea. Akifungua kuanza
kwa uzalishaji huo rais wa Ghana John Atta Mills alisema "kuzalishwa kwa
mafuta hayo ni baraka na siyo laaana kwa wananchi wa Ghana, na mafuta yatakayo
patikana yataisaidia Ghana kuinua uchumi wake zaidi kulio ilivyo sasa."
Kiasi cha mapipa 55.000 yanatarajiwa kuzalishwa kwa siku. Eneo hilo
liligunduliwa kuwa linamafuta miaka mitatu iliyo pita na kampuni moja ya
Uingreza Tullow Oil PLC. Picha hapo juu ni ya ramani ya nchi ya Ghana ikiwa
imefunikwa na rangi za bendera ya nchi hiyo ambayo kwa sasa inatambulika rasmi
kuwa mzalishaji wa mafuta na kujiungana na nchi nyingine zilizopo katika bara
la Afrika. Wanasiasa
maarufu Kenya wahusishwa katika machafuko ya 2007
Nairobi, Kenya - 15/12/2010. Mwanasheria mkuu wa mahakama ya
kimataifa ya makosa ya jinai ametangaza rasmi majina ya watu walioshukiwa
kuhusika na machafuko wakati na kabla uchaguzi mkuu uliofanyika 2007.
Moreno Ocampo, alitangaza majina
hayo "Uhuru Kenyatta ambaye ni waziri wa fedha, William Ruto, Fransis
Muthaura, Joshua Arap Sango mwandishi wa habari, Henry Kosgey na mkuu wa polisi
wa zamani Mohamed Hussein."
Akiongea mara baada ya kumaliza kutaja
majina hayo, Moreno alisema watu hawa washukiwa hawa bado hawana makosa mpaka
hapo mahakama itakapo wakuta na hatia.
Uamuzi huo wa mahakama ya kimataifa
kuingilia kati swala hilo la kutafuta ukweli ni watu gani walikuwa vinara wa
kuongoza machafuko ulikuja kutokana na serikali ya Kenya kuchukua muda
kuwatambua watu hawa waliotajwa.
Picha hapo juu ni ya bendera ya
Kenya nchi ambayo ilikuwa na machafuko makubwa ya kihistoria katika nchi hiyo
tangu kupata uhuru kutokana na mvutano wa kisiasa na itikadi zilizopo kati ya
wananchi wake.
Mahakama
ya kubali maombi ya dhamana ya Julian Assange. London,
Uingereza Mahakama jijini London imekubali kumwachia kwa masharti
mwanzilishi wa mtandao wa Wiki Leaks kwa dhamana ya dola za Kiamerika $
317,400.
Julian Assange 39,ambaye
anashitakiwa nchini Sweden kwa kosa la kufanya mapenzi ya kustukiza ambayo
nimakosa nchini Sweden. Assange alijipeleka mwenyewe polisi mara ya karatasi ya
kutaka kukamatwa kwake kutolewa na Interpol baada ya serikali ya Sweden
kumfungulia mashitaka. Hata hivyo upo uwezekano wa serikali ya Sweden kupinga
rufaaa hiyo. Picha hapo juu anaonekana Julian Assange ambaye anashukiwa na
makosa ya kufanya mapenzi ya kushtukiza na moja ya mwanadada hivi karibuni
nchini Sweden. Wanasheria
wa Kenya wafikiria mara mbili mkataba wa Roma. Nairobi,Kenya -
14/12/2010. Kundi la wanasheria nchni Kenya wametishia kuandika barua kwa bunge
la Kenya kufuta uanachama wake katika Mahakama ya Kimataifa (International
Criminal Court-ICC). Kundi hilo la wanasheria walisema " tulitaka haki
itendeke na mahakama ya kimataifa lakini haikuwa hivyo kutokana na uchunguzi
wao. Na tunaangalia ni njia gani tutatumia kupitia bunge kujitoa katika
matakaba wa Roma ( RomeStatute)." Mjadara huo umekuja baada ya ICC kusema
inamajina sita ya watu waliohusika kuleta machafuko ya kisiasa kabla na baada
ya uchaguzi mkuu uliofanyika 2007. Machafuko hayo yalisababisha vifo vya watu zaidi
ya 1500 na wengine 300,000 kuachwa bila makazi. Picha hapo juu anaonekana mmoja
wa kijana akikimbia kuepusha maisha yake kutokana na machafuko yaliyo tokea
kabla na baada ya uchaguzi nchini Kenya 2007 ambapo hali ya kiusalama ilikuwa
imechafuka, kutisha kwa kilahali. Waziri mkuu wa Itali ashinda kura za maoni kwa mara
nyingine. Roma, Itali -
14/12/2010. Waziri mkuu wa Itali ameshinda kura za maoni ambazo zilikuwa
zimeitishwa zidi yake kutokana na baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali
kutokwa na imani naye. Silvio Berlusconi,ameshida kura hizo za maoni kwa kiasi
cha uchache wa kura dhidi ya wale wanaopinga uongozi wake. Ushindi huo aliopata
Berlusconi, siyo wa mara ya kwanza kwani alishida kura kama hiyo siku za nyuma.
Hata hivyo wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema Berlusconi atakuwa na wakati
mgumu kuongoza serikali kutokana na upinzani mkubwa katika bunge na serikalini.
Picha hapo juu anaonekana waziri mkuu wa Itali,Silvio Berlusconi akionyesha
dole baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa kuwa ameshinda tena kura za maoni
ambazo ziliitishwa na vyama vya upinzani hivi karibuni. Dunia ya mpoteza mtetezi wa amani.
Washington, Mshauri mkuu wa serikali ya Amerika
katika maswala na hali halisi ya nchi za Pakistan na Afghanistan amefariki
dunia baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo kwa mara ya pili.
Habari kutoka Ikulu ya Amerika
zimesema "Richard Holbrooke 69 alikuwa amelazwa katika hospital ya rufaa
George Washington kwa ajili ya matibabu mara baada ya kupata matatizo ya
moyo."
Rais wa Amerika Baraka Obama alisema
" ameshutushwa na kifo cha Richard Holbrooke, na alikuwa mwananchi
mwaminifu aliyependa nchi yake na kuitumikia kwa hali na mali, wanachi wa
Amerika tomepoteza shujaa ambaye alikuwa mlinzi na mtetezi wa Amerika katika
nyanja za kimataifa na kuhakikisha amani inapatikana kwa hali na mali."
Richard Holbrooke, alikuwa kinara
katika kutetea na kuleta amani hasa katika nchi za Ulaya ya Mashariki
zijulikanazo kama nchi za Balkans, pia kutumia mbinu zote kusimamisha vita vya
Bosnia na alikuwa ni mmoja wa washauri wa rais Obama katika vita vinavyo
endelea nchini Afghanista ili kujadili mbinu za kukabidhi madaraka kwa
Waafghanistan.
Picha hapo juu anaonekana marehemu
Richard Holbrooke, akiongea katika moja ya mikutano ya kimataifa enzi za uhai
wake.
Waziri
mkuu wa Itali kuwekwa kenye boksi la maoni na wabunge. Roma, Itali -
12/12/2010. Wachunguzi wa serikali wameanza uchunguzi kufuatia kuwepo na habari
ya kuwa waziri mkuu wa Itali ametoa milungula ili ashinde kura za maoni kuuhusu
uongozi wake. Malalamiko hayo yalifunguliwa na kiongozi wa upinzani Antonia Di
Puerto ambaye akikosoa uongozi wa waziri mkuu wa sasa Silvio Berluscon. Naye
kiongozi mwingine wa chama cha upinzani Luigi De Magistris alisema
"tumeona rushwa inatumika kati ya wabunge ili kumuunga mkono
Berluscon." Hata hivyo Berluscon alisema "sidhani kama kutakuwa na
wasaliti wengi na naimani serikali itashinda." Uamuzi wa kutaka kura za
maoni zipigwe kumekuja kutokana na baadhi ya wabunge hasa wa upande wa upinzani
kutokuwa na inami na waziri mkuu kutokana na habari za matukio ambayo
yanamuhusisha moja kwa moja. Picha hapo juu ni picha waziri mkuu wa Itali,
Silvio Berluscon ambaye serikali yake imekuwa na mvutano sana na vyama pinzani
na kutaka kura za maoni zipigwe zidi ya uongozi wake.
Uchaguzi
wa wabunge Misri waleta mvutano upya.
Kairo, Misri - 12/12/2010. Mamia ya watu wameaandamana kupinga
matokeo ya uchaguzi wa wabunge kwa kudai ya kuwa haukuwa wea haki na kutaka
mwanasheria mkuu kufuta matokeo.
Katika matokeo hayo chama tawala
kinacho ongozwa na rais Housein Mubarak kimeshinda kwa kupata vitu vingi katika
bunge. Naye msemaji wa mmoja wa chama cha upinzani George Ishak alisema
"watu wanaandamana kupinga matokeo hayo na tutapinga kwa kufungua kesi ili
kuonyesha ya kuwa uchaguzi haukuwa wa halali." Kufuatia matokeo hayo
Mohamed ElBaradei aliyekuwa mkuu wa maswala ya Atomi amevitaka vyama vya
upinzani kupinga kwa pamoja kushiriki katika uchaguzi wa urai uanaotarajiwa
kufanyika mwaka ujao. Picha hapo juu wanaonekana polisi wa kuzuia ghasia wakiwa
wanawazuia wananchi walioandamana mbele ya mahakama kuu kutoleta maafa na
kuhakikisha usalama na amani unakuwepo.
Japana kuweka mitambo ya kuzuia mashambulizi ya anga. Tokyo, Serikali ya Japan inajiandaa kuweka mitambo ya kuzuia
Japana kuweka mitambo ya kuzuia mashambulizi ya anga. Tokyo, Serikali ya Japan inajiandaa kuweka mitambo ya kuzuia
mashambulizi ya anga kutokana na
kukua kwa mgogoro katika eneo zima la Asia Pasifiki. Habari zilizo patikana
zinasema "mitambo aina ya Patriot Advavced Capabilty 3 itawekwa
kuzuia mashambulizi ya anga pindipo kutatokea mashambulizi." Kitendo cha
serikali ya Japan kuamua kuweka mitambo hiyo kinakuja kutokana na matukio ya
Korea ya Kaskazini kuishambulia Korea ya Kusini hivi karibuni, jambo ambalo
limezidi kuleta myumbo na mashaka katika eneo hilo la Asia Pasifiki. Picha hapo
juu inaonekana moja ya mitambo ya kijeshi ambayo serikali ya Japan ina mpango
wa kuiweka mitambo ya kivita ilikuzuia mashambulizi yoyote ya anga pindipo
yatakapo fanyika. Wabunge
wapinga malipo ya kiafya ya Septemba 11.
Washington,
Amerika 12/12/2010. Wabunge wa chama cha Republikan nchini Amerika wamepinga
mswaada wa serikali kutaka kutoa malipo ya huduma za kiafya kwa wale wote walio
athirika wakati wa mashambulizi ya Septemba 11/2001. Kwa mujibu wa habari
zilizo patikana zinasema "kukataliwa kwa maswaada huo wa kuwasaidia malipo
ya kiafya kutawaathiri pia wafanyakazi waliokuwa wanafanya kazi katika eneo
hilo na wakazi wa vitingoji vya karibu na Ground Zero." Tangu tukio
la Septemba 11/2001, wanasiasa wamekuwa wakipishana kimawazo kuhusu swala hili.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika harakati za
kusafisha mabaki ya majengo yaliyo bomoka, mara baada ya kulipuliwa na ndege
zilizo tekwa nyara na magaidi.
Bomu lalipuka katikati ya jiji la Stockholm.
Stockholm, Maofisa wa upelelezinchini Sweden
wameanza rasmi kuchunguza tukio la bomu ambalo lililipuliwa katikati ya jiji la
Stockholm jana.
Anders Thornberg ambaye ni afisa wa
upelelezi alisema "tumeanza uchunguzi wa tukio hilo na tunalichukulia kama
ni la kigaidi."
Katika mlipuko wa bomu hilo watu
walijeruhiwa kutokana na mlipuko huo uliotokea jana wakati baadhi ya watu
wakiwa mbioni kununua vitu kwa ajili ya kujianda na sherehe za Krismas
Hata hivyo shirika la habari la
Sweden lilipata email iliyokuwa imeeleza kuwa huenda kukatokea tukio hilo
kutokana na Sweden kujishirikisha katika vita vya Afghanistan na kitendo cha
mchoraji mmoja raia wa Sweden kuchora picha ya kumkashifu Mtume Mohamed S.W.A.
Picha hapo juu wanaonekana
wafanyakazi wa zima moto wakiwa wanazima moto uliotokana na mlipuko wa bomu
kabla ya kuleta maafa makubwa.
Ujeruman
na Ufaransa zasema tutailinda sarafu ya Euro.
Freiburg, Kansela wa Ujerumani na rais wa Ufaransa wamekuta mjini
Freiburg kujadili njia mbadala za kuimarisha sarafu ya Ulaya (EURO). Kansela
Angela Markel na Nikolas Sarkozy walikutana na kuangalia kiundani njia ambazo
zitaifanya sarafu ya Euro kuimarika zaidi hasa katika wakati uhu mgumu wa
myumbo wa uchumi duniani. Viongozi hao kwapamoja walisema "tuta ilinda
Eoro, kwani ni sarafu ya Euro ndiyo Ulaya yenyewe."
Kukutana kwa viongozi hao kunakuja
kabla ya mkutan wa viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Ulaya kufanyika
siku chache zijazo. Picha hapo juu anaonekana rais wa Ufaransa Nikolas Sarkozy
kushoto akiongea huku Kansela Angela Markel akimsikiliza kwa makini sana na
kutathmini nini hasa anaongea wakati walipo kutana hivi karibuni kujadili nini
la kufanya ili sarafu ya Euro kuwa imara zaidi kimataifa. Zawadi ya Nobel yawekwa kwenye kiti
cha mtarajiwa.
Oslo, Norway -10/12/2010. Sherehe za kumzawadia mshindi wa
zawadi ya amani ya Nobel mwaka 2010 imefanyika jijini Oslo bila ya mzawadiwa
kuwepo. Liu Xiaobo ambaye ni raia na mazaliwa wa China ndiye aliyekuwa mshindi
wa zawadi ya amani ya mwaka 2010, lakini hakuweza kuudhulia sherehe hiyokwani
anatunikia kifungo cha miaka 11 jela kwa kosa la uhani kwa mujibu wa sheria za
China. Hata hivyo zawadi yake iliwekwa kwenye kiti ambacho alitarajiwa kukalia
wakati wa kupokea zawadi hiyo. Thorbjoern Jagland ambaye ni mwenyekiti wa
kamati hiyo ya kutoa zawadi alisema " Liu hajafanya kitu au jambo baya
yeye ni mwanaharakati wa kutetea haki za binadamu." Msemaji wa serikali ya
Chini Jiang Yu, alimesema "kutolewa kwa zawadi hiyo kwa Liu ni siasa iliyo
shinikiza, ambayo ni zao la wakati wa vita vita vya baridi, na hivyo China
haitakukubali kuingiliwa katika maamuzi yake." Picha hapo juu wanaonekana
wageni waalikwa wakiangalia picha ya Liu Xiaobo aliye tunikiwa zawadi ya amani
ya Nobel 2010 lakini hauwepo kwenye sherehe hizo na zawadi yake kuwekwa kwenye
kiti alicho tarajiwa kukikalia.
Mwanzilishi
wa mtandao wa Wiki Leaks awekwa kizuizini
London, Mahakama ya jijini London
imemkatalia dhamana mwanzilishi wa mtandao wa Wiki Leaks ambaye alijipeleka
mwenyewe polisi.
Julian Assange 39, aliwasili kwenye
kituo cha polisi na baadaye kufikishwa mahakamani kutokana na kesi ya kufanya
mapenzi ya kushutukiza iliyofunguliwa juu yake nchni Sweden.
Mwanasheria wa serikali wa Sweden
aliomba mahaka kutompa dhamana Julian Assange kwa kuwa hajulikani
anapoishi."
Hata hivyo mwanasheria Mark
Stephens,ambaye anamwakilisha Julian Assange alisema " tutakata rufaa siku
ya Jumanne wiki ijayo na ikiwezekana tutaenda mahamaka kuu na nina amini ya
kuwa mahakama ya Uingereza itataua swala hili bila matatizo. "
Picha hapo juu ni ya Julian Assange
ambaye mtandao wake umetikisa ulimwengu wa siasa na wa kidiplomasia baada ya
kuchapisha habari za siri.
Waziri
mkuu wa Uingereza afanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan.
Kabul, Afghanistan - 07/12/2010. Waziri mkuu wa Uingereza amefanya
ziara ya ghafla nchini Afghanistan na kukutana na rais wa nchi hiyo.
Waziri mkuu David Cameron, aliongea
mbele ya waandishi wa habari alisema " uhusiano wa wanchi wa Afghanistani
na Uingereza utazidi kudumishwa na jumuiya ya kimataifa ishirikiane kuijenge
Afghanistan."
Hata hivyo David Cameron, aliongezea
kwa kusema " natumaiini hali itazidi kuwa nzuri na itaturuhusi kuanza
kufikiria kuondoa majeshi yetu ifikikapo mwakani."
Kabla ya kuongea na rais Hamid
Karzai, David Cameron alitembelea wanajeshi wa Uingereza waliopo katika jimbo
la Helmond.
Picha hapo juu anaonekana waziri
mkuu wa Uingereza David Cameron kushoto akiwa na mwenyeji wake rais wa
Afghanistan Hamid Karzai kulia wakati walipo kuwa wakiongea na waandishi wa
habari.
Urussi
kuwa mwanachama wa World Trade Organazations 2011.
Brussels,
Ubelgiji - 07/12/2010. Jumuiya ya Ulaya imekubali na kuunga mkono kwa Urussi
kuwa nchi mwana chama World Trade Organizatio, (WTO) ifikapo mwaka 2011.
John Clancy mbaye ni msemaji wa
jumuiya ya Ulaya alisema "tumetia sahihi mkataba huo na Urussi baada ya
kufikia maafikiano kwa pamoja."
Kukubaliwa huko kwaUrussi kuwa
mwanachama wa WTO kutainua kwa kiasi kikubwa uchumi kati ya nchi wanachama na
inakakadiliwa kufika kiasi cha asilimia 3.3 na hata kuongezeka katika siku za
mbele.
Picha hapo juu wanaonekana viongozi
wa Urussi na jumuiya ya nchi za Ulaya wakiwa katika mkutano ili kujadili nini
cha kufanya ili kudumisha uhusiano wa karibu.
Mazungumzo
ya kinyuklia na Iran bado kitendawili.
Geneva,Uswis -
07/12/2010.Mkutano wa mazungumzo kati ya Iran na nchi za jumuia ya Ulaya, nchi
wanachama wa kudumu wa kamati ya usalama ya umoja wa Mataifa
Urussia,China,France, Uingereza,
Ujerumani na Amerika umekwisha bila lengo la mkutano huo kufikiwa.
Saeed Jalili ambaye ni mkuuwa wa
maswala ya kinyuklia ya Iran,alisema "hatutazungumzia maswala ya maendeleo
yetu ya kinyuklia na uzalishaji wake katika kikao kijacho amabcho kinatarajiwa
kufanyika Instambul nchini Uturuki na kuhusu swala hilo basi lazima kuwepo na
ushirikiano kutoka pande zote mbili."
Naye mmoja wa wajumbe toka Amerika
alisema "matarajio ya mkutano wetu hayakufikiwa na kuleteta matoke
finyu."
Dhumuni la mkutano huo, ilikuwa ni
kuzungumzia hali halisi ya maswala ya kinyukli yanavyoendeshwa nchini Iran,
lakini hakuna ufumbuzi uliofikiwa.
Picha hapo juu anaonekana Saeed
Jalili mkuu wa maswala ya kinyuklia wa Iran, akitoka katika ukumbi wa mkutano,
mara baada ya kumaliza mazungumzo.
Mazungumzo
ya Iran na Umoja wa Mataifa yaanza nchini Uswisi.
Geneva, Uswis - 06/12/2010. Shirika linalo simamia na kudhibiti
uzalishaji nishati za kinyuklia limeanza mazungumzo na serikali ya Iran ili
kujadili mpango mzima wa kinyuklia uliopo nchini Iran. Mazungumzo hayo ambayo
yameudhuliwa na viongozi wa jumuiya ya Ulaya,Urussi, Amerika, Uingereza, China
na Ujeruman nchi wanachama katika kamati ya baraza la usalama la Umoja wa
Mataifa, wataongelea kiundani na kujadili na serikali ya Iran kuhusu undeleaji
wa mpango mzima wa nyuklia.
Picha hapo juu anaonekana Saeed
Jalili kiongozi kutoka serikali ya Iran anaye shughulikia mswala ya nyuklia
kulia akiongea na mkuu wa maswala ya mambo ya nje wa jumuiya ya Ulaya Cathirine
Ashton kabla ya kuanza mazungumzo.
Argentina
yaunga mkono kuwepo kwa taifa la Palestina.
Buenos Aires,
Argentina -06/12/2010. Serikali ya Argentina imefuatia msimamo wa Brazil kwa
kukubali kuunga mkono kuwepo kwa Taifa la Wapalestina walio huru.
Katika barua iliyo tumwa kwa rais wa
Wapalestina Mohmoud Abbas na uongozi wa Argentina ilisema " tunaitambua
Palestina kama taifa huru kutokana na makubaliano ya mipaka ya mwaka
1967."
Kuungwa mkono huko kwa serikali ya
Wapalestina na nchi za Amerika ya Kusini umekuwa wakaribu sana hasa katika
kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Picha hapo juu anaonekana rais wa
Wapalestina Mahmoud Abbs akisalimiana na rais wa Argentina Cristina Kirchner
wakati walipo kutana katika moja ya mikutano kujadili hali halisi ya
Wapalestina.
Mmiliki wa
ndege za Konkodi atozwa faini.
Paris,France - 06/12/201. Shirika la ndege lilio kuwa mmiliki wa
aina ya ndege Concorde limetozwa faini baada ya kukutwa na hatia ya
kuhusika na kutokuwajibika katika usalama wa ndege hiyo ambayo iliungua moto.
Shirika hilo Continental Air
lines lilitozwa faini kiasi cha $ US dollor 268,400 na mahakama nchini Ufaransa
baada ya ndege yake aina ya Concorde kushika moto wakati inaanza kupaa
na kuanguka na kupoteza maisha ya abiria 113.
Picha hpo juu ni ya ndege ya aina ya
Concorde ikiwa imeshika moto mara baada ya kuanza kupaa.
Sunday,
December 5, 2010
Umoja
wa Afrika watuma mjumbe kuleta suruhu za kisiasa nchini Ivory Coast. Abidjan,Ivory
Coast - 05/12/2010. Rais wa pili wa Afrika ya Kusini tangu kushindwa kwa
utawala wa kibaguzi wa rangi, Thabo Mbeki amewasili jijini Abidjan ili kuleta
suruhisho la matokeo ya uchaguzi wa rais. Kwa mujibu wa habari zilizo patikana
zinasema "Thabo Mbeki ameteuliwa na Umoja wa Afrika (UA) kushughulikia
swala la matokeo ya uchaguzi wa Ivory Coast, ambapo rais mtetezi Laurent Gbagbo
waliapishwa kuwa rais, ingawaje apo awali kamati ya uchaguzi ilimtangaza
mpizani wake Allasane Ouattara kuwa mshindi kwa kupata kura nyingi zaidi."
Kuwasili huko kwa Thabo Mbeki kunatarajiwa kuleta suruhisho ili kuepuka mvutano
wa kisiasa. Uchaguzi nchini Ivory Coast uliwahi kuhairishwa zaidi ya mara tano
kutokana na mvutano wa kisiasa. Picha hapo juu ni ya aliyekuwa rais wa Afrika
ya Kusini Thabo mbeki, ambaye anatarajiwa kuleta suruhisho la kisiasa nchini
Ivory Coast.
Jeshi la Umoja wa Afrika kuwa na wakati mgumu.
Mogadishu,
Somalia - 05/12/2010. Kundi la Al-Shabab lililopo nchini Somalia limesema
litaendelea kupambana na majeshi ya wageni waliovamia nchi yao.
Maelezo hayo yalitolewa na mmoja wa
kiongozi wa wapiganaji kwa kusema " wamevamia nchi yetu na hatuna budu
kuitetea."
Kwa mujibu wa shirika la kutetea
haki za binadamu zinasema "zaidi ya watu mia moja wamefariki katika
kipindi cha miaka mitatu tangu kuanza mapambano kati ya Al-Shabab na jeshi la
UA ."
Picha hpo juu wanaonekana wanajeshi
wa Umoja wa Afika wakiwa katika mazoezi ya kijeshi ili kupambana na kundi la
Al-shabab.
Picha ya pili ni ya kundi la
Al-Shabab kundi ambalo limekuwa ilikiendeleza mashambulizi zidi ya wanajeshi wa
umoja wa Afrika na raia ambao wanakwenda kinyume na Al-Shabab.
Iran
yatangaza kuzalisha madini ya kinyuklia.
Tehran, Serikali ya Iran imetangaza ya kuwa
wanasanyansi wake wameweza kuzalisha kwa mara ya kwanza madini ya ambayo
yanatumika katika kuzalisha nguvu za nyuklia.
Akiongea mkuu huyo wa maswala ya
kinyuklia Ali Akbar Salehi alisema "Iran itaanza kutumia madini yake hayo
kwa mara ya kwanza ambayo yamezalishwa hapa nyumbani na kutotegemea kuagiza
toka nchi za nje."
Kitendo cha Iran kutangaza uwezo
wake huo, kutazidi kuleta vichwa kuuma kwa Amerika na nchi nyingine ambazo
haziamini ya kuwa Iran haina mpamgo wa kutengeneza siraha za kinyuklia.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya
wanasayansi wa Irani wakiwa kazini katika kiwanda cha kuzalishia nguvu za
kinyukli.
Wamisri
wapiga kura tena kuwachagua viongozi wao.
Kairo,Misri -
05/12/2010. Wanachi wa Misri wamepiga kura kwa mara ya pili ili kuwachagua
wabunge.
Uchaguzi huo wa mara ya pili wa
kuchagua wabunge unafanyika huku vyama vya upinzani vikiwa vimejitoa kwa
kupinga ya kuwa uchaguzi huo si harali.
Uchaguzi huo ambao chama tawala
(NDP)-National Democratic Party) kinatarajiwa kushinda viti vingi kutokana na
kujitoa kwa vyama vya upinzani.
Picha hapo juu wanaonekana baadhi ya
wadau wa vyama vya upinzani wakiwa wametawanywa na polisi wa kuzuia ghasia
wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa awali.
Baraka
Obama afanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan. Kabul,
Afghanistan - 03/12/2010. Rais wa Amerika amefanya ziara ya ghafla nchini
Afghanistan na kuongea na wanajeshi na raia wa Amerika wanaoshiriki kwa katika
vita zidi ya Taliban na washirkia wake. Akiongea katika hotuba hiyo rais Baraka
Obama alisema "Amerika itaendelea na kupambana na wale wote ambao
wanapinga maendeleo ya Amerika au kutishia usalama wa Amerika na watu wake, na
hatutashindwa kamwe kuwasaka popote walipo." Hata hivyo katika ziara hiyo
rais Baraka Obama, hakuweza kukutana na rais wa Afghanistan kutokana na hali ya
hewa kuwa mbaya. Picha hapo anaonekana rais wa Amerika Baraka Obama akishuka
kutoka kwenye ndenge mara baada ya kuwasili nchini Afghanistan kwa mara ya pili
akiwa kama rais wa Amerika ili kuwapa salamu za sikuku wanajeshi na kuelezea ni
kwa jinsi gani Waamerika wote wapo pamoja nao. Ulaya ya kumbwa na mporomoko wa
barafu. London, Uingereza
- 03/12/2011. Bara la Ulaya limekumbwa na mporomoko wa barafu ambao
umesababisha hali ya utoaji wa huduma kuyumba. Barafu hizo ambazo zinaendelea
kugubika karibuni Ulaya kote tokea Urussi hadi Spain limekuwa gumzo kwa wakazi
wengi wa eneo hili. Siku ya Jumanne barafu nyingi ilipolomoka na kusababisha
hali ya hewa kuwa barisi hadi kufikia kati ya hasi 20 na 22. Picha hapo juu
linaonekana moja ya gari la kusafisha njia likijaribu kutoa barafu ili huduma
ziweze kuendelea zilishindikana kutokana na wingi wa barafu iliyo poromoka toka
angani
Subscribe to:
Posts (Atom)