Friday, January 31, 2014

INDIRA GANDHI




Leo hii niko hai pengine kesho inawezekana nisiwe hapa. Nitaendelea kuwatumikia wananchi wa India mpaka pumzi yangu ya mwisho. Na kama nikifa,kila tone la damu yangu litajenga muungano usiofutika.


Hayo ni baadhi ya maneno ya waziri mkuu wa kwanza mwanamke wa India, bibi Indira Ghandi katika hotuba yake ya mwisho,siku moja  kabla ya kuuawa, oktoba 30 mwaka 1984. Hoja nyingi zilijengwa ndani na nje ya ya india baada ya hotuba yake ya mwisho,huku wengi wakiyatafsiri maneno yake kama utabiri wa kifo chake siku moja baadae.




Uzito wa maneno hayo ulitimia siku moja baadaye,kwani alipoteza maisha kwa shambulio la risasi kutoka kwa walinzi wake. Oktoba 31 mwaka 1984,walinzi wawili wa Gandhi,Satwant Singh na Beant Singh,walimfyatulia risasi mwanamama huyo wakati akitembea kwenye bustani yake iliyopo barabara ya 1 Safdarjung Road,New Delhi.



Gandhi alipigwa risasi wakati akielekea kwenye mahojiano na mcheza filamu wa England, Peter Ustinov,ambaye lengo la mahojiano hayo ilikuwa ni kuandaa kipindi maalumu documentary. Singh alifyatua risasi tatu kwa Ghandhi huku mwenzake Satwant akifyatua risasi zisizofahamika idadi. 





Baada ya kuhakikisha wamekamilisha mauaji,walinzi hao walijisalimisha. Baada ya hapo walipelekwa kwenye chumba maalumu kwa ajili ya kuhojiwa, ambapo Bent Singh alipigwa risasi,huku mwenzake akihukumiwa adhabu ya kunyongwa kwenye jela ya Tihar. 





Uchunguzi wa mwili wa Gandhi uliofanywa kwenye kituo cha sayansi na tiba,india alikopelekwa baada ya kuondolewa sehemu ya tukio,ulithibitisha kifo chake kutokea baada ya kupigwa risasi 30 sehemu mbalimbali mwilini.




 Gandhi alitangazwa amefariki dunia saa 10 baadaye,ingawa taarifa za awali zilidai kuwa alifariki siyo zaidi ya dakika moja baada ya kushambuliwa kwa risasi. Kuna sababu nyingi zimeelezwa zikihusishwa na kifo cha Gandhi,





lakini kubwa inayotajwa ni chukio la kundi la uasi la Kalasinga la mjini Punjab,India lililochukizwa na uamuzi wa Gandhi kuamuru jeshi liwashambulie. 






Inadaiwa kuwa Gandhi alitoa amri kwa jeshi kuvamia hekalu la kalasinga walikokuwa wamejificha waasi wenye silaha,na baada ya shambulizi kufanyika haukupita muda mrefu Gandhi akauawa na walinzi wake. 




Indira Gandhi alizaliwa November 19 mwaka 1917. Ni waziri Mkuu wa kwanza mwanamke nchini India. Indira alizaliwa kama binti wa Jawaharial Nehru,aliyekuwa waziri mkuu wa kwanza wa India kati ya mwaka 1947 hadi 1964. 



Jina la Gandhi alipokea kwa njia ya ndoa na Feruz Gandhi ambaye hakuwa na uhusiano na Mahatma Gandhi. Alishirikiana na baba yake kama karani katika shughuli zake za kisiasa na ilipofika mwaka 1955, alikuwa mwenyekiti wa chama tawala cha congress. 



Baada ya kifo cha baba yake, mzee Nehru aliingia katika serikali kama waziri, na baadaye akachaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1966 akatawala hadi 1977 mwaka 1980 alirejea madarakani tena na kushika uongozi wa juu,na ni katika kipindi hicho ulipotokea uasi uliosababisha kukosekana kwa amani kabla ya kuamuru nguvu ya jeshi kutumika,. Siku chache baada ya kuuawa,mtoto wake wa kiume Rajiv Gandhi,akatawazwa kuwa waziri mkuu kuanzia mwaka 1984 mpaka 1989 alipouawa kwa bomu la kutegwa.




No comments:

Post a Comment